DAKTARI ALIYEIBA WATOTO AHUKUMIWA CHINA

Daktari mmoja katika mkoa wa Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuwaiba watoto saba ku...

Daktari mmoja katika mkoa wa Kaskazini wa Shanxi nchini Uchina amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuwaiba watoto saba kutoka hospitali aliyokuwa akihudumu na kuwauza watoto hao kwa wauzaji watoto.

Hukumu hiyo ya kifo hubadilika na kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili ya mshitakiwa kubadili tabia.

Wakati mmoja daktari Zhang Shuxia alikuwa mtaalam mashuhuri lakini sasa ni nuhalifu mwenye hatia aliyejipatia faida kubwa kutokanana na uuzaji wa watoto.

Daktari huyo aliwadanganya wazazi wapya kwamba watoto wao walizaliwa wakiwa na ugonjwa mbaya.Aliwahadaa kwamba iwapo wazazi wangeliwachia serikali jukumu la kuwaangalia basi wangepewa matibabu ya hali ya juu waliohitaji.

Watoto hao wenye afya njema baadaye waliuzwa kwa bei ya maelfu ya madola kwa wauzaji watoto wanaohudumu katika mikoa ilio karibu.

Sita kati ya watoto walioibwa walipatikana na kurudishwa kwa wazazi wao huku mtoto mmoja aliyeuzwa kwa dola 165 pekee akipatikana ameaga dunia kandokando ya barabara ambapo alikuwa ameachwa na muuzaji mmoja wa watoto.
BBC

Related

JESHI LA POLISI LAFUKUZA WANNE

Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Kamishina Suleman Kova akizungumza na wanahabari muda huu ofisini kwake juu ya kufukuzwa kwa askari hao. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaa...

BABA ATUHUMIWA KUMMUA MWANAYE WA MIAKA 8

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Na Edwin Moshi, Njombe Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa...

TAZAMA PICHA: NYUMBA ZA JESHI LA POLISI ZILIVYOTEKETEA KWA MOTO TANGA

  Nyumba za Askari wa jeshi la polisi zilizopo eneo la chumbageni nyuma ya kituo kikuu  cha polisi cha chumbani jijini Tanga zaliungua moto.  Mh.Halima Dendegu akishuh...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904769
item