RAIS KIKWETE ATEUA MAKATIBU TAWALA WAPYA MIKOA MITANO NA KUHAMISHA WENGINE WAKIWEMO WAKURUGENZI WA MAJIJI
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/rais-kikwete-ateua-makatibu-tawala.html
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumamosi, Januari 18, 2014, amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wapya wa mikoa mitano na kuhamisha makatibu tawala wengine na Wakurugenzi wa Majiji nchini.
Taarifa
ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue iliyotolewa jioni ya
leo, Ikulu, Dar Es Salaam inasema kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza
leo hii.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, Makatibu Tawala wapya ni Ndugu Wamoja A.
Dickolangwa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa
ambako alikuwa Kaimu Katibu Tawala; Ndugu Abdallah D. Chikota ambaye
ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya hapo, alikuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Newala na Ndugu Symthies E.
Pangisa ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya
uteuzi wake, Ndugu Pangisa alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Wengine
ni Ndugu Alfred C. Luanda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
wa Mtwara. Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Tabora na Ndugu Jackson L. Saitabau ambaye ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Kabla ya hapo, alikuwa Katibu Tawala
Msaidizi wa Mkoa wa Arusha.
Taarifa
hiyo iliwataja waliohamishwa kuwa ni Ndugu Beatha Swai aliyekuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Pwani na sasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu,
TAMISEMI; Ndugu Sipora J. Liana ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la
Arusha anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI; Ndugu Benedict Ole
Kuyan ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga anahamishiwa Mkoa wa
Mara na Ndugu Salum M.Chima ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Rukwa anahamishiwa Mkoa wa Tanga.
Wengine
waliohamishwa ni Ndugu Mgeni Baruani ambaye alikuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Njombe anahamishiwa Mkoa wa Pwani; Ndugu Juma R. Iddi ambaye
alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya anahamishiwa Jiji la Arusha kama
Mkurugenzi; Eng. Omari Chambo ambaye alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya
Uchukuzi anahamishiwa Mkoa wa Manyara kama Katibu Tawala wa Mkoa huo na
Dkt. John Ndunguru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi
anahamishiwa Mkoa wa Kigoma kama Katibu Tawala wa Mkoa huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Januari, 2014