TAPELI WA KIKE ALIYETAPELI KWA NJIA YA AIRTEL MANOY AFUNGWA KIFUNGO NZEGA MKOANI TABORA, AWATAPELI MAWAKALA FEDHA KWA NJIA YA MTANDAO.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa hapa kwenda jela miezi sita, kwa kosa la utapeli wa fedh...


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa hapa kwenda jela miezi sita, kwa kosa la utapeli wa fedha kwa njia ya mtandao wa Airtel Money kwa mawakala mbalimbali wilayani humo.
Akitoa hukumu hiyo, Hakim Mkazi Mfawidhi, Joseph Ngomelo, alisema mshitakiwa Helena Alexandria, atakwenda jela miezi sita baada ya kukiri kufanya utapeli huo.

Mshitakiwa huyo alikiri kutapeli mawakala mbalimbali wa Airtel Money waliopo Nzega mjini kwa njia ya mtandao na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Alisema kifungo cha mama huyo kitakuwa fundisho kwa wanawake wangine wenye tamaa, kwani makosa kama hayo yakiachiwa yanaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Polisi Mkaguzi Msaidizi, Melito Ukongoji, aliiambia Mahakama hiyo kuwa Januari mosi mwaka 2014, mshitakiwa ambaye ni mkazi wa Nzega mjini, aliiba kwa kutumia mtandao wa Kampuni ya Airtel Money.

Alidai kuwa Hellena alikuwa akitumia ujumbe mfupi wa maneno wenye muamala wa kutoa pesa Sh 40,000 Airtel Money na kujipatia Sh 40,000 kwa kila wakala kwa nyakati tofauti.

Akijitetea, mshitakiwa alikiri kuhusika na tuhuma hizo kwa nyakati tofauti na kuongeza kuwa lengo lilikuwa ni kutafuta fedha za kujikimu kimaisha kutokana ugumu wa maisha.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo Mwendesha Mashitaka aliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo za wizi wa utapeli kwa njia ya mtandao.
HABARI LEO

Related

KONGAMANO LA UIMBAJI KWA VIJANA KUTOKA MAJIMBO MBALIMBALI YA KKKT DAR ES SALAAM LILIOFANYIKA TAREHE 15/06/2013 USHARIKA KWA KIJITONYAMA

Kongamano hili lilijumuisha kwaya 18 ambazo ni: KIPUNGUNI B KIBANGU CHARAMBE KIMANGA  YOMBO DOVYA MBEZI BEACH KEKO YOMBO VITUKA WAZO HILL MWENGE MAVURUNZA MTAA WA NEEMA MAGOMENI ...

UTOAJI WA TUZO ZA BONGO MOVIE 2012-2013 KATIKA PICHA

WAZIRI WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MAKAME MBAWALA AKIFUNGUA TUZO HIZO JACOB STEEVEN, JB - MSANII BORA WA KIUME MZEE MAJUTO - MSANII BORA WA UCHEKESHAJI STEVE NYERERE ...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO KINATOA RAI KWA WATANZANIA KULAANI HILA NA NJAMA CHAFU ZINAZOENDESHWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA CHAGUZI NDOGO ZA MARUDIOChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904763
item