SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KATIKA PICHA
Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani na gari la wazi kwenye ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/sherehe-za-maadhimisho-ya-miaka-50-ya.html
Rais wa Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia
kwenye uwanja wa Amani na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50
ya Mapinduzi.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya
wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Amani kwenye kilele
cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Uganda
Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya viongozi waandamizi wa
Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi. |
Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi "Mapinduzi Daima".
Rais wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride
kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa
Amani.
Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Maandamano mbali
mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za Serikali
yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar na
viongozi wengine.
Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari
wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa
wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi cha
Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha
za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.