TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wana...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/taarifa-kwa-umma-kuhusu-tuhuma-dhidi-ya.html
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU TUHUMA DHIDI YA
MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE
Kama
mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama
ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa
Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote
zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi
anayoiongoza;
Tuhuma hizo
ni pamoja na;
1. Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM),
Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni
katika jimbo hilo.
2. Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono
alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo
wa Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa.
3. Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu
Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili
ya kampeni za mgombea urais.
4. Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi
mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam
Aziz kwa ajili ya kampeni.
Idara ya
Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;
1. Hakuna ukweli hata mmoja katika
tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu
wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana
tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba
matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya
ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho
kimepoteza ushawishi kwa wananchi.
2. Matokeo ya uongo huo ni kutaka
kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.
3. Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda
kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa
CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa,
ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua
hatua za kisheria.
4. Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii
ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda
mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali
popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa
waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.
5. Tungependa kuwaambia waliozusha
tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika
jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti
dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu
masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na
viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu,
ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya
kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.
6. Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika
mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli
zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika.
Imetolewa leo Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA