MKURUGENZI WA BODI YA UTALII AFUTWA KAZI

Dkt. Aloyce Nzuki Wizara ya maliasili na Utalii imemfuta kazi mkurugenzi wa bodi ya utalii Tanzania dokta Aloyce Nzuki kwa kutokuw...


Dkt. Aloyce Nzuki

Wizara ya maliasili na Utalii imemfuta kazi mkurugenzi wa bodi ya utalii Tanzania dokta Aloyce Nzuki kwa kutokuwa na imani nae pamoja na utendaji usioridhisha.
Hii imekuja baada ya kikao cha pamoja kati ya Bodi hiyo na waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ambao waliketi pamoja na kutathmini utendaji kazi ya Mkurugenzi huyo.
Waziri NYALANDU amekiri kupokea Changamoto kadhaa zinazokwamisha ufanisi wa majukumu ya Bodi ya Utalii katika kusimamia Sekta hiyo na kusema ‘mimi na Naibu waziri wangu nimeridhika na kuridhia kuondolewa kazini kwa Aloyce Mzuki’
Kwenye sentensi nyingine Waziri Nyalandu amesema ‘sisi kama Wizara tutampangia kazi nyingine, vilevile nimeiagiza bodi ya utalii Tanzania waitangaze nafasi ya Mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii nchini’
Mwingine aliezungumza ni mwenyekiti wa bodi hiyo Balozi Charles Sanga aliesema sekta ya utalii inahitaji mabadiliko makubwa katika kufikia azma ya Serikali ya kuongeza idadi ya watalii nchini kuliko taifa lingine lolote barani Afrika.
Kwa sasa nafasi hii ya mkurugenzi itakaimiwa na Devotha Mdachi ambae ni mkurugenzi wa masoko katika bodi.

Related

OTHER NEWS 1036983440345588009

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item