BENKI YA DUNIA KUINYIMA UGANDA MSAADA
Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria mpya d...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/benki-ya-dunia-kuinyima-uganda-msaada.html
Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa
Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha
sheria mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini
yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika
sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .
Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini
Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja.
Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha
misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza
kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.
Asilimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden,
akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na
wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu
kuwa sheria yoyote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa
muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza
kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
BBC
BBC