CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE
Benson Kigaila akiongea na wanahabari Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujib...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/chadema-watoa-siku-tatu-kwa-rais-kikwete.html
Benson Kigaila akiongea na wanahabari
Rais
Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha
unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi
ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa jumuiya za
kimataifa.
Rais
Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu
ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Chadema
wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga amani ndani ya nchi.
Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.
“Kauli
aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana na vitendo vinavyofanywa na
viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga amani nchini,” alisema na
kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.
Mkurugenzi
wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa Rais
Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia
jana, vinginevyo watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa
kama sehemu ya malalamiko yao.
Alisema
kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na alihoji kwanini awatake
WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala ya kuacha hatua za
kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo ni polisi na
majeshi na mahakama.