RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitor...

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) jana February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia niWaziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ProMakame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ProfJohn Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) jana February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua jana February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ProfJohn Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.

  
Dar es Salaam. 
 Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha mchakato wa Sheria ya Usalama kwenye mitandao unakamilika na kuanza kutumika, ili kudhibiti wanaotoa siri za nchi kwa kisingizio cha uhuru wa habari.
Hayo aliyasema jana kwenye hafla ya uzinduzi wa mtambo maalumu wa usimamizi na uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, (TTMS), iliyofanyika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Dar es Salaam.
Rais Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani ambayo haitunzi siri zake, kwa kuwa jambo hilo ni muhimu kiusalama, hata kwa mataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wa vyombo vya habari.
Alisisitiza kwa kumtolea mfano aliyekuwa Jasusi wa Marekani, Edward Snowden, anatuhumiwa kuvujisha siri za nchi hiyo kwenye mtandao, ambaye sasa amekimbilia mafichoni Urusi. Aliwapongeza TCRA kwa hatua hiyo, akieleza kuwa inawezesha uchumi wa nchi kupata kichocheo cha kukua kwa kuwa sasa kutakuwa na udhibiti wa mawasiliano hasa ya simu za nje ya nchi na kuongeza kipato kwa taifa.
Awali Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema kufungwa kwa mitambo hiyo, kunakwenda pamoja na kuwapo kwa kanuni mpya za mawasiliano ya usimamizi na uhakiki wa mawasiliano ya simu (TTMS, Regulation 2013), ambapo imewezesha Serikali kupata senti 7 kati ya 25 zinazotozwa kwa kila dakika na nyingine zinagawanywa kwa kampuni husika.
“TCRA imefanikiwa kuilipa Hazina mgawo wa mwezi Oktoba, kwa mujibu wa Sheria ya TMMS Sh1.6 bilioni, leo tutakabidhi malipo ya Sh1.6 bilioni malipo ya Novemba hatimaye mwezi Machi tutalipa ya Desemba,” alisema Nkoma.

Mwananchi

Related

OTHER NEWS 8054589325813071085

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item