VURUGU ZA WAKULIMA MOROGORO, MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA
Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wameshika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiy...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/vurugu-za-wakulima-morogoro-mabomu-ya.html
Wananchi
wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wameshika mawe
na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wakitaka
Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.
Askari
wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima Moto uliowashwa na wakulima
waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao
walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro Dk Joel Bendera Ili kutatua Mgogoro uliopo kati ya
wakulima na wafugaji uliopo katika vijiji hivyo.Askari wa jeshi la
Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya Machozi mara baada ya Wananchi wao
kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na
Mkuu Wa Wilaya ya mvomero.
Askari
wa Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza
Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya.
MOROGORO
Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela,
Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa -
Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende
kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.
Wakulima wa kijiji cha Mangae wilaya Mvomero wamefunga barabara kuu ya
Morogoro. Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la
Mkangazi baada ya wananchi kuvamiwa na kupigwa wakulima hao
walikusanyikajana usiku na kufikia maamuziWakulima hao wanadai kuwa
wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na
kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika
Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo
wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha mgongamano mkubwa
wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao
walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa. Baada ya vurugu kuwa
kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile
aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na
kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya
machozi na kufanikiwa kuwatawanya.Wananchi takribani 20 wamekamatwa na
polisi katika vurugu hizo. Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari
yameanza kupita eneo hilo.