Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akiwaisili Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam, tayari kuzindua w...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/waziri-kawambwa-azindua-rasmi-taarifa.html
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akiwaisili Hoteli ya Double Tree jijini
Dar es Salaam, tayari kuzindua warsha ya uwasilishaji wa ripoti ya
upimaji wa Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa
la pili iliyofanyika mwezi wa Oktoba 2013 kwa ufadhili wa serikali ya
Marekani kupitia Shirika la USAID. Katikati ni Naibu Waziri wa TAMISEMI
Kassim Majaliwa na Kulia ni Mkurugenzi wa USAID Tanzania Sharon Croner.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu
wa Shirika la USAID Tanzania Bw, David Bruns akielezea jijini Dar es
salaam matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika lake kuhusu upimaji wa
Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili
iliyofanyika nchini Oktoba mwaka jana kwa ufadhili wa serikali ya
Marekani na taarifa yake kuzinduliwa rasmi jijini Dra es salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (Katikati) akiteta jambo na Naibu Waziri wa
Tamisemi Kassim Majaliwa (wa pili kutoka kulia) wakati wa uzinduzi wa
Warsha ya uwasilishaji ripoti ya upimaji wa wa Kitaifa wa Stadi za
kusoma ,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika mwezi wa
Oktoba 2013. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Profesa Sifuni Mchome. Wengine kutoka Kushoto ni Kamishina wa
Elimu Profesa Eustela Bahalalusesa na kulia ni Mkurugenzi wa USAID
Tanzania Sharon Croner waliofanya utafiti huo
Mkurugenzi wa Shirikala la
USAID Tanzania Sharon Croner, akiongelea jijini Dar es salaam matokeo ya
utafiti uliofanywa na Shirika lake wakati wa uzinduzi wa Warsha ya
uwasilishaji waripoti ya upimaji wa Kitaifa wa Stadi za kusoma
,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika Oktoba mwaka jana.
Taarifa ya utafiti huo ilizinduliwa jana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Shukuru Kawabwa(Katikati) Naibu Waziri wa Tamisemi (Elimu)
Kassim Majaliwa (wa pili kulia ) Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kulia) Kamishna wa Elimu
Tanzania Profesa Eustela Bahalalusesa (kushoto ) na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la USAID Tanzania Bi, Sharon Croner wakifuatilia uwasilishwaji
wa taarifa mbalimbali wakati wa warsha ya uzinduzi wa uwasilishaji
ripoti ya upimaji wa Kitaifa wa Stadi za kusoma ,Kuandika na Kuhesabu
kwa darasa la Pili iliyofanyika mwezi wa Oktoba mwaka jana
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akiongea wakati wa uzinduzi wa Warsha ya
uwasilishaji waripoti ya upimaji wa wa Kitaifa wa Stadi za kusoma
,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika Oktoba mwaka jana
na serikali ya Marekani kupitia shirika lake la Maendeleo la USAID
Tanzania ,jana katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
USAID Tanzania Bi, Sharon Croner wakati wa uzinduzi wa Warsha ya
uwasilishaji wa ripoti ya upimaji wa Kitaifa wa Stadi za kusoma
,Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la pili iliyofanyika Oktoba mwaka jana
na shirika la maendeleo la Marekani la USAID Tanzania ,jana katika
Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Naibu
Waziri wa Tamisemi Kassim Majaliwa .Warsha hiyo iliwashirikisha wadau
mbalimbali wa elimu hapa nchini.
Baadhi ya wadau wa Elimu
kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini wakifuatilia uzinduzi wa Warsha ya
uwasilishaji wa ripoti ya Upimaji wa Kitaifa wa Stadi za
Kusoma,Kuandika na Kuhesabu kwa Darasa la Pili uliofanyika jijini Dar
es Salaam jana. Utafiti huo ulifanywa na Shirika la Misaada la Marekani
la USAID kwa ufadhili wa Marekani.
Tanzania Imepiga hatua kubwa katika kuyafikia malengo ya Milenia ya
kuhakikisha utoaji wa elimu ya msingi kwa watoto wote ifikapo mwaka 2015
ambapo kwa sasa, uandikishaji wa watoto wote katika elimu ya msingi
umefikia asilimia 96.2.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam
na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa wakati
akifungua warsha ya uwasilishaji wa ripoti ya upimaji wa kitaifa wa
Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu maarufu KKK kwa darasa la pili
uliofanyika mwezi Oktoba 2013.
Hata hivyo Waziri Dkt Kawambwa
amesema matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la
UWEZO mwaka 2010 yanaonesha kwamba zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi
katika madarasa ya chini hawazimudu stadi za Kuandika, Kusoma na
Kuhesabu kwa kiwango kinachotakiwa.
"Ni hakika kwamba,
ufundishaji wa stadi za Kuandika, Kuhesabu na Kusoma unatakiwa ufanyike
kwa makini hata hivyo upo ushahidi kwamba ufundishaji huo haufanyiki
kama ilivyotarajiwa."Alisema Dkt Kawambwa
Amesema hali hiyo ya
ufundishaji hafifu inajidhihirisha zaidi kwa matokeo ya ufaulu wa chini
katika madarasa ya juu darasa la nne la saba.
Waziri Dkt
Kawambwa amesema Ili kutatua changamoto hiyo na kuwezesha kuinua
kiwango cha ubora wa elimu itolewayo,, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi kwa kiushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imeanza kutekeleza mkakati wa Matokeo
Makubwa Sasa, (Big Results Now )
Amesema chini ya utekelezaji
wa Makkati wa Matokeo Makubwa sasa katika sekta ya elimu upimaji wa
kitaifa wa stadi za KKK na mafunzo kazini kwa walimu wa darasa la I
& II kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi hizo ni miongoni mwa
mikakati 9 iliyoibuliwa.
Aidha Waziri huyo wa Elimu nchini
ameishukuru serikali ya Marekani ambayo kupitia shirika la USAID,
imewezesha kufanya upimaji wa kitaifa wa stadi za KKK ulioongozwa na
taasisi ya "Research Triangle Institute"(RTI).
"Ni matarajio
yangu kwamba matokeo ya upimaji huu uliofanyika kwa kutumia Zana za
"Early Grade Reading Assessment (EGRA)", the "Early Grade Mathematics
Assessment (EGMA)" na "Snapshot of School Management Effectiveness
(SSME)" utaisaidia serikali kupata taarifa kuhusu hali halisi ya
kumudu stadi za KKK kwa wanafunzi wa Darasa la Pili."Alisema
"Matokeo ya utafiti huu pia yatasaidia katika kulinganisha na matokeo
ya upimaji wa darasa la pili unaotarajiwa kufanyika mwaka 2014 na 2015
pamoja na kusaidia serikali katika kuandaa programmu mbalimbali ili
kufikia malengo tarajiwa ya kuinua ubora wa elimu na ufaulu"Aliongeza
.
Ushiriki wa Jamii na Wazazi katika masuala ya elimu ni muhimu ili
kuinua upatikanaji wa elimu bora, upatikanaji wa rasilimali na kuongeza
uwajibikaji.
Tanzania ina rekodi nzuri ya ushirikishaji wa
jamii kupitia kamati za shule na taasisi za kiraia na hivyo Waziri Dkt
Kawambwa ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau mbalimbali wa elimu
kuwasaidia watoto kwa kuwawezesha kupata na kutumia stadi mbalimbali za
lugha kupitia usomaji wa vitabu na kuzungumza nao wakiwa nyumbani ili
hatimaye kuwawezesha kufanya vizuri wakiwa shule.