BARABARA YA KIMARA - KIVUKONI KUMALIZIKA NDANI YA MIEZI 6 KUANZIA SASA

Kampuni ya Strabag International  inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaa...

Kampuni ya Strabag International  inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa  inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza.
 
Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit – BRT) ambao umeelezewa kuwa una changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu.
 
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwa kazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.
 
Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280.
 
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
 
Waziri Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyokusudiwa. “Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo wake” alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara kinyume na sheria.
 
Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu. “Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa visingizio vya kutokamilika kazi hii kwa wakati” ametahadharisha Mhe. Magufuli.
 
Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara  hiyo upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa eneo kati ya Ubungo na Kimara.
 

Related

OTHER NEWS 64598044966010106

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item