SITTA ATANGAZA MAJINA YA WENYEVITI NA MAKAMU WENYEVITI KAMATI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Dodoma Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo (jana), ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kama...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/sitta-atangaza-majina-ya-wenyeviti-na.html
Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo (jana),
ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge
hilo.
Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo baada ya uchaguzi wa
viiongozi hao uliofanyika (jana) Machi 24 , mwaka 2014 mjini Dodoma .
Mwenyekiti ametangaza majina haya baada ya kuunda kamati hizo jana kwa
mujibu wa kanuni ya 54 (1) ya kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014
ambazo zimetungwa chini ya kifungu cha 26 (1) cha sheria ya Mabadiliko
ya Katiba sura ya 83, ambazo zinataja kuundwa kwa kamati 12 za Bunge
Maalum.
Wenyeviti na makamu wenyeviti waliochaguliwa katika kamati hizo ni
pamoja na Kamati ya Uandishi ambayo Mwenyekiti amechaguliwa
Mhe. Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma.
Kamati ya Kanuni
Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba.
Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni Prof.
Makame Mbalawa.
Wengine waliochaguliwa katika Kamati Na. 2 ni Shamsi Vuai Nahodha
ambapo Makamu wake ni Shamsa Mwangunga, Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni
Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma Mussa Juma.
Mhe. Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni
Christopher Ole-Sendeka, Makamu wake ni Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati
Na. 5 Mwenyekiti ni Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni Assumpter
Mshama.
Waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti ni Stephen Wassira na
Makamu wake ni Dkt. Maua Daftari, Kamati Na. 7 Mwenyekiti Brig.
Hassan Ngwilizi ,Makamu wake Waride BakariJabu, Kamati Na. 8
Mwenyekiti ni Job Ndugai,Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.
Hali kadharika Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh, Makamu
wake Wiliam Ngeleja, Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu
wake ni Salmin Awadh Salmin, Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni Anne
Malecela, Makamu wake Hamad Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti
niwake Paul Kimiti na Makamu wake ni Thuwaybah E. Kisasi.
Aidha, kwa uchaguzi huo, Mhe. Sitta alitangaza wajumbe wa Kamati ya
Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba ambao ni wenyekiti wote wa kamati
hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua kwa mujibu wa Kanuni.
Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni pamoja
na Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba,
Amon Mpanju na Hamoud Abuu Juma. Hata hivyo pamoja na majina hayo
kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na kujitoa katika nafasi hiyo hivyo
kufanya nafasi za uteuzi kuwa nne badala ya Tano .