NDEGE YA MALAYSIA ILIYOTOWEKA HAIJAPATIKANA
Maafisa wa Idara ya usafiri wa ndege wa Malaysia Wakati juhudi za kuisaka ndege iliyopotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Malaysi...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/ndege-ya-malaysia-iliyotoweka.html
Maafisa wa Idara ya usafiri wa ndege wa Malaysia
Wakati juhudi za kuisaka ndege iliyopotea ilipokuwa ikisafiri kutoka
Malaysia kuelekea Uchina zikiendelea, ndege moja ya Vietnam imeripoti
kuwa imeona kitu kinachofanana na mlango wa ndege kwenye ufuo wa bahari
ya Kusini mwa Uchina kwenye mwambao wa taifa hilo.
Hata hivyo hakuna thibitisho kuwa mlango huo ni wa ndege iliyopotea ya
Malaysia, iliyokuwa na abiria mia mbili na thelathini na tisa.
Uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kupotea kwa ndege hiyo mapema
siku ya Jumamosi, inawalenga abiria wawili wanaodaiwa kuwemo ndani ya
ndege hiyo, waliotumia paspoti iliyoibiwa.
Stakabadhi hizo mbili za kusafiria kutoka Italia na nyingine Australia inaaminika kuibwa nchini Thailand.
Idara ya polisi ya Kimataifa, Interpol, inasema kuwa ni mapema mno kuhusisha pasi zilizoibwa na kutoweka kwa ndege hiyo.
Na huku kushughuli za kuisaka ndege hiyo
zikiendelea, Msemaji wa shirika la ndege la Malysia amewaambia jamaa ya
watu waliokuwemo katika ndege hiyo, kujiandaa kwa taarifa mbaya.
Amesema kufikia sasa hakuna mawasiliano yoyote na ndege hiyo masaa 30 sasa tangu itoweke.
Wakuu wa Malysia wanasema jumla ya meli 30 na
ndege 44 kutoka mataifa tisa tofauti duniani, yamejiunga katika shughuli
za kuitafuta ndege hiyo.
Kamanda William Marks wa kikosi cha saba cha
jeshi la wanamaji la Marekani, ametuma ndege aina ya USS Pinckney
kusaidia katika usakaji huo.
''Jambo la kwanza kufanywa ni kukadiria mahala
na kwa sasa tunalenga mawasiliano ya mwisho kutoka kwa ndege hiyo kabla
ya kutoweka na mawasiliano ya rada. Kutoka hapo tunahesabu mwendo kasi
ya upepo na mawimbi. Kutoka hapo tunagawanya na eneo na tunatafuta
kutumia kila kifaa tuliyonayo- na hiyo siyo tu kutumia vifaa kutoka
Marekani lakini pia kutumia meli na anga kutoka mataifa mengine ya
dunia." Alisema kamanda huyo.
Ameonya kuwa shughuli hiyo ya kutafuta ndege hiyo inakumbwa na changamoto nyingi.