TAARIFA KUHUSU UKAGUZI WA LESENI ZA BIASHARA

  Afisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara Nicodemus Mushi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa l...

 Afisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara Nicodemus Mushi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa leseni za biashara kwenye ukumbi wa MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa waizara hiyo Christopher Mashingo.Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO), Frank Mvungi.

Hussein Makame-MAELEZO
WIZARA ya Viwanda na Biashara imewataka wananchi kufuata sheria na taratiu za nchi katika kuendesha biashara zao kwani kufanya hivyo ni alama ya maendeleo na  kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu ni  jinsi anavyofuata taratibu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uhamasishaji wa Masoko wa wizara hiyo, Christopher Mashingo wakati akizungumza na waandishi wa habari ukaguzi wa leseni za biashara leo jijini Dar es Salaam.
Mashingo alisema Serikali ilirejesha utaratibu wa kupata leseni ya biashara kwa kulipia kuanzia Julai 1 mwaka jana na kutoa kipindi cha miezi 6 kwa wafanyabiashara waliokuwa na leseni zisizo na ukomo kuhuisha leseni zao.
Alisema kipindi hicho kiliisha Desemba 31 mwaka na wale waliochelewa kufanya hivyo walipata leseni zao kwa kulipa ada na adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Leseni Namba 25 ya mwaka 1972 kifungu cha 11 (a) na (b).
“Wito kwa wananchi kufuata kufuata sheria na taratiu za nchi katika kuendesha biashara zao kwani kufanya hivyo ni alama ya maendeleo na  kigezo kimoja cha kupima maendeleo ya watu ni  jinsi anavyofuata taratibu”, alisema Mashindo.

Alisema ofisi yake inafanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za nchi kama alivyoagiza Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara.
Aliongeza kuwa Katibu Mkuu huyo aliagiza kwamba Mamlaka za Leseni zifanye ukaguzi wa kina katika maeneo yao, na kusisitiza kuwa ukaguzi huo ufanyike kati ya mwezi April na Mei.

Related

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KWA MAFANIKIO BARIADI, ASEMA WAPINZANI WAJIPANGE 2015

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari  wa shina namba 12 tawi la Isenge kata ya Dutwa. Katibu Mkuu...

KWA RIPOTI HII UWEZEKANO WA KINA MASOGANGE KUACHIWA HURU NI MKUBWA

WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kua...

KOSA LA NDUGAI

  HUKU akijitapa kuwa ndiye mlinzi wa kanuni za Bunge, na akiwalaumu wabunge, hasa wa upinzani, kwa kukiuka kanuni hizo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amebainika kuwa alivunja kanuni nyi...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item