VIJANA WATATU WAKAMATWA NA KETE ZA MADAWA YA KULEVYA, NYAYA YA TTCL MKOANI LINDI.
Watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi Renatha Mzinga Baadh...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/vijana-watatu-wakamatwa-na-kete-za.html
Watuhumiwa wakiwa mikononi mwa polisi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi Renatha Mzinga
Baadhi ya madawa waliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Salum Shaban Mapande
Nyaya zilizokamatwa kwa mtuhumiwa Abdul Mahamud ambazo zimeyeyushwa zinasadikiwa kuwa za kampuni ya simu(TTCL)
Na Abdulaziz Video, Lindi
Watu watatu wanashikiliwa na Polisi Mkoani Lindi kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin pamoja na Miundo mbinu ya Kampuni ya simu kinyume na Sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi Renatha Mzinga amesema leo (jana) kuwa kwa ushirikiano mkubwa waliopewa na wanajamii wamefanikiwa kumkamata Bw Salum Shaban Mapande(32)Mkazi wa Dar es sallam akiwa na madawa ya kulevya kete 42 kubwa na ndogo 104 zenye uzito wa Gram 58 na pesa taslim tsh 2,827,500 zinazosadikika kuwa za mauzo ya madawa hayo.
Watumiwa wengine waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha Utalii mjini Lindi, Masudi Mohamed(19) aliekutwa na kete 35 za bhangi huku Abdul Mahamud na Halfan Salum waliokutwa na nyaya za kampuni ya simu TTCL Zenye Uzito wa kg 5.
Kamanda Mzinga alisema mkoa wa Lindi umeanza kampeni kubwa ya kupambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo kupambana na wimbi la uingizaji na uuzaji wa madawa ya kulevya ambalo kwa sasa kuna ongezeko kubwa la utumiaji na uuzaji wa madawa hayo ikiwemo pombe haramu ya gongo.
Aidha Kamanda Mzinga ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujidhatiti na kufichua wahalifu wakiwemo wauza madawa ya kulevya ambapo Jeshi lake litatoa ushirikiano na usiri kwa watakaotoa taarifa zinazoashiria Uvunjifu wa Amani ikiwemo za Usalama barabarani