BASI LA A.M COACH LAPATA AJALI ENEO LA IPULI NA KUSABASHA KIFO CHA MWANAFUNZI MMOJA

  Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya   Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika en...

 Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya
 Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo.

 Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika  kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu
 Askari Polisi Kitengo cha usalama barabarani wakiuchukua mwili wa mtoto aliyegongwa na basi la kampuni ya A.M maeneo ya Ipuli Mnadani ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza,katika ajali hiyo watu kadhaa wamejeruhiwa.
Wananchi wakishuhudia mwili wa mtoto aliyegongwa na basi hilo ambapo walishauri Serikali iliifungie kampuni hiyo ya A.M Coach kuleta mabasi mkoani Tabora ambayo walidai kuwa ni mabovu na yanausalama mdogo kwa wasafiri.

TABORA
Kufuatia kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya kampuni ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga marufuku mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si salama kwa wasafiri na wapita njia.

Wananchi hao ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la Ipuli mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda shuleni kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la A.M Coach lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.

Aidha wananchi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya kampuni hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana kuyumba barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu za mkoa wa Tabora.


Wameitahadharisha Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima.

Related

OTHER NEWS 4557580993037853038

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item