BUNGE MAALUM LA KATIBA LAONGEZEWA SIKU 60

Mwenyekiti wa Bunge Maalum wa Katiba, Mh. Samwel Sitta Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba limeomba kuongezewa muda wa siku 60 kuanzia ...

Mwenyekiti wa Bunge Maalum wa Katiba, Mh. Samwel Sitta
Dodoma.
Bunge Maalumu la Katiba limeomba kuongezewa muda wa siku 60 kuanzia Agosti 5, mwaka huu litakapokutana kwa ngwe ya pili, Mwananchi limebaini.
Bunge hilo linahitimisha ngwe yake ya kwanza Aprili 25, mwaka huu likiwa limekutana kwa siku 67, kati ya 70 zilizokuwa zimetengwa awali.
Kwa muda huo wa ziada 60, iwapo wajumbe wote 629 watalipwa posho ya Sh300,000 iliyopangwa kwa siku, jumla ya Sh11.322 bilioni za walipakodi zitatumika ukilinganisha na Sh13.209 bilioni zilizotumika katika siku 70 za awali. Jumla ya fedha zote zitakazotumika kwa posho ni Sh24.53 bilioni, bila kuingiza gharama nyingine nje ya posho za wajumbe.
Jana, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alitangaza kwamba shughuli za Bunge hilo zitakoma wakati wajumbe wake watakapokwenda kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano, Aprili 26, mwaka huu.
Sitta alisema jana kwamba aliwasilisha maombi ya kuongezewa muda kwa Rais Jakaya Kikwete, ambayo yalikuwa hayajajibiwa.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipoulizwa jana alisema: “Mheshimiwa Rais (Kikwete) anachoafiki ni kama ambavyo kila mtu anaona mwenendo wa Bunge ulivyo, kwamba siku 70 haziwatoshi, hivyo alikubali kwamba wanahitaji kuongezewa muda. Ingawa mpaka sasa hajaamua atawaongezea siku ngapi, atakapoamua tutawafahamisha tu.”
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema upo uwezekano mkubwa wa Bunge hilo kuongezewa siku 60 lakini akaongeza kuwa hilo litategemea bajeti itakayoidhinishwa na Serikali.
“Kwa kuwa kazi hii ndiyo kwanza iko katika hatua zake za kwanza, ndiyo maana mchakato wake umesogezwa mbele mpaka Agosti mwaka huu,” alisema Jaji Werema.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema: “Mwenyekiti hajanipa taarifa rasmi kwamba tutakutana kwa siku ngapi, ila ninachofahamu ni kwamba tunasubiri barua rasmi kutoka kwa Rais.”
Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, nyongeza ya muda wa kukutana kwa Bunge hilo inatolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar.
Hamad alisema tayari Sitta alishawasilisha maombi ya kuongezewa siku za Bunge hilo kukutana, lakini akasema hana hakika kama majibu tayari yamerejeshwa.
Hamad alisema wakati Bunge litakapoahirishwa litakuwa limebakiza siku tatu, ambazo zitafidiwa wakati watakapokutana Agosti 5.

Related

BUNGE NA SONGOMBINGO LAKE KATIKA PICHA, HALI INATISHA

SEHEMU NAMBA MOJA. Hapa askari wa bunge wakipambana na mhe Joseph Mbilinyi huko mhe akiwa ameshika mkono wa kipaza sauti kufuatia kutoelewana ndani ya ukumbi wa bunge jana WATU AAAH, MSHANG...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara. Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa ...

HUYU NDIE MWANAMKE ALIYEKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA JNIA

Huyu ndiye mwanamke aliyekamatwa na kete za madawa ya kulevya akiwa chini ya ulinzi.  Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Nige...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item