MAJAMBAZI YAUA POLISI DAR ES SALAAM (SAMAHANI KWA PICHA)
Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke Mwili wa jambazi mwingine ukiwa...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/05/majambazi-yaua-polisi-dar-es-salaam.html
Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke
Source: Matukio Blog
Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira.
Mwili wa askari polisi ukiwa umepakiwa kwenye gari ya polisi tayari kupelekwa hospitali ya Temeke kuhifadhiwa.
Askari
polisi mmoja wa kituo cha polisi Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa
Temeke, ameuawa kikatili siku ya ijumaa mchana baada ya kupigwa risasi
ya kifua na majambazi waliokuwa wanajaribu kutoroka baada ya kufanya
tukio la kihalifu. Askari hao waliokuwa doria katika eneo la Wailes
walijikuta wakishambuliwa kwa risasi na majambazi hao mara baada ya
majambazi hao kujaribu kukimbia katika eneo la tukio kwa kutumia usafiri
wa pikipiki kipindi ambapo askari polisi walikuwa karibu na eneo la
tukio. Hata hivyo wakati askari hao wakijaribu kuwafukuza majambazi hao
wawili kwa lengo la kuwakamata ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na
kumpiga risasi ya kifua askari huyo na kufariki pale pale.
Hata
hivyo katika harakati za kujaribu kukimbia majambazi hao walianguka na
pikipiki waliyokuwa wakitumia ndipo wakaamua kutimua mbio mitaani na
kuingia katika nyumba moja ambapo walijificha na kujifanya kama ni
wakazi wa eneo hilo, baada ya wnanchi na polisi kufika katika nyumba
hiyo, baadhi ya majirani waliwaambia polisi kwamba wameona watu hao
wameingia katika nyumba hiyo. Baada ya polisi kuingia waliwakuta watu
hao wakiwa wametulia kama kwamba wao ni wakaazi wa nyumba hiyo na wala
hawajui lililotokea.
Baada ya kuwatambua watu hao,
polisi waliwatia nguvuni huku wananchi wenye ghadhabu waking'ang'ania
kuwa wanataka kuwaua sababu wameshaua askari mmoja. Baada ya vuta
nikuvute kati ya wananchi na askari hao ambao walikuwa wachache,
wananchi walifanikiwa kuwachukua majambazi hao kwa nguvu kutoka mikononi
mwa polisi na kuanza kuwapiga kwa silaha mbalimbali za kienyeji
yakiwemo mawe na marungu mpaka watuhumiwa hao wakapoteza maisha.