SERIKALI YATOA TAMKO: MATIBABU YA DENGUE NI BURE
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Said Meck Sadiki, amewataka wananchi wa mkoa huo wanapohisi wana dalili za ugonjwa wa dengue kuwenda ka...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/05/serikali-yatoa-tamko-matibabu-ya-dengue.html
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Said Meck Sadiki, amewataka wananchi wa mkoa huo wanapohisi wana dalili za ugonjwa wa dengue kuwenda katika hospitali za Serikali kwa kuwa matibabu hutolewa bila malipo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kuulizwa swali juu ya gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa
huo, kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares
Salaam.
“Tunaomba
wananchi wanapohiisi dalili za ugonjwa huo kwenda katika hospitali za
Serikali ,ambazo ni Amana, Mwananyamala na Temeke kwa kuwa matibabu
yanatolewa bila malipo” alisema Sadiki.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi,leo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema vituo vyote vya Serikali vinapaswa
kutoa matibabu ya ugonjwa huo bila malipo kwa kuwa ugonjwa huo ni
mlipuko na magonjwa ya milipuko matibabu yake hutolewa bila malipo.
Mwamwaja
pia alisema ikitokea hata vituo vya afya vya binafsi vikapewa
vitenganishi na vifaaa vya tiba na Serikali navyo vinasapwa kutoa
matibabu ya ugonjwa huo bila malipo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa wanajenga uwezo ili kila wilaya iwe na vituo vitano kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa huo.
Sadick
aliongeza kuwa Serikali itanyunyuzia dawa ya (Lavacide) sehemu za
mikusanyiko kama vile mashulenina kwenye madimbwi, lakini maeneo ya
hotelini na mabaa watapaswa kunyunyuzia dawa kwa gharama zao.
“ Kwa
upande wa wizara, idara na taasisi za Serikali wanapaswa kunyunyuzia
dawa kwa gharama zao,(yaani matumizi mengineyo)” alisisitiza huku
akisema hata kwenye ofisi yake wamefanya hivyo kwa gharama zao.
Aidha
Sadiki aliwataka viongozi wa mitaa na watendaji wengine kuwahimiza
wananchi kuhusu usafi wa mazingira ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa
huo.
Alisema
wananchi wanapaswa kuhakikisha vifuu vya nazi visoda kwani maji kidogo
yanayokaa katika vitu husababisha mbu wanaosabbaisha ugonjwa huo
kuzaliana , hivyo vinatakiwa visitupwe ovyo na kufunika maji safi
wanayoyahifadhi.
Alisisitiza hatua ya kwanza kuzuia ugonjwa huo ni usafi wa mazingira,hivyo dawa ni hatua ya mwisho.