CCM, CHADEMA NUSU WAZIPIGE KAVUKAVU KWENYE MKUTANO DAR ES SALAAM

  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na ...

  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana.


  Wafuasi wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika  akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla  akihutubia katika mkutano huo.
   Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada hani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
 Naibu Waziri wa Maji, Ammos Makalla na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), wakitofautiana jukwaani wakati Makalla akiamuru polisi kuwatoa wafuasi wa Chadema waliokuwa wakimzomea wakati akileleza Utakelezaji wa Ilani ya CCM juu ya maji, Huku Mnyika akitaka waendlee kuzomea akidai kwamba Waziri hakufanya haki kwani yeye alipokuwa akizomewa na wana CCM hakuwachukulia hatua katika mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Mavuruza, Kata ya SalangaAmos Makalla

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, EvaSinare (katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.
   Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema
   Mbunge wa Jimbola Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo
   Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa  jiji la Dares Salaam kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi wake umeanza sasa.
 Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.
 Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutano uliofanyika Kata ya Kibamba.
 Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo
 Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dares Salaam, (Dawasco), Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa maji katika kata hiyo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Related

OTHER NEWS 8287090395935139720

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item