MAOFISA 13 UWANJA WA NDEGE WAFUKUZWA KAZI

Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi akitoa ufafanuzi wa kufukuzwa kwa wafanyakazi 13 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwl. Nye...

Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi akitoa ufafanuzi wa kufukuzwa kwa wafanyakazi 13 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwl. Nyerere.

Zaidi ya Maofisa kutoka wizara tatu wapato 13 waliokuwa wakifanya kazi katika uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere, wamerudishwa katika wizara zao kwa kosa la kupokea rushwa kwa wageni wanaoingia kutoka nchi mbalimbali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Uchukuzi Dr. Herrison Mwakyembe alisema kuwa, maofisa hao walikuwa katika kitego cha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Afya na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Wageni ambao walikuwa wanakaguliwa na kuobwa rushwa na wafanyakazi hao ni kutoka nchini China, India na Nchi za Kiarabu, ambao wakifika uwanjani hapo wanakaguliwa mabegi kama amebeba dawa za asili dawa hizo huchukuliwa na maofisa wa kilimo na baadae kuobwa pesa na kurudishiwa dawa hizo.
Pia kama ameingia hajachoma sindano ya homa ya manjano anaamriwa na kuulizwa kwanini hujachoma na akioneakana anakaidi anaambiwa atowe chochote kitu kisha anaachiwa, hivyo hivyo kwa upande wa uvuvi na mifugo nako wanafanyiwa hivyo.

Kufuatia malalamiko hayo ya wageni wanaoingia hapa nchini, wageni hao waliamua kuyapeleka kwa Waziri Mwakyembe, naye bila ya kusita aliunda tume ambayo iliangalia kamera za usalama na kupata maofisa 13 waliobainika kufanya uchafu huo, ambao unachafua taswira ya nchi yetu na kuwakimbiza wawekezaji.

Related

TUJUZANE 7027954506512902629

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item