UDA WAPAKA RANGI KUONYESHA RUTI ZA DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Maendeleo ya UDA, Henry Bantu. Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kuanzia jana wameweka stika za...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/uda-wapaka-rangi-kuonyesha-ruti-za-dar.html
Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Maendeleo ya UDA, Henry Bantu.
Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kuanzia jana wameweka stika za
rangi kwa pamoja na vibao kwa mbele ambayo vinaonesha, gari linaelekea
wapi kwa hapa jijini.
Akizungumza na Taarifa News Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na
Maendeleo ya UDA, Henry Bantu alisema kuwa zoezi hilo la kuweka stika za
rangi litasaidia kuwaonesha abiria mbalimbali mabasi hayo yanaelekea
wapi.
Bantu alisema kuwa hapo awali mabasi hayo yalikuwa hayana vibao wa
stika ya rangi mbele kwa kuonesha basi linaelekea wapi, lakini kwa sasa
hakuna tatizo kila abiria atajua basi hilo linaelekea wapi kwa rangi
ambayo ataiona mbele pamoja na vibao.
Aidha alizitaja rangi hizo kuwa ni jani la mgomba rangi hiyo
inawakilisha njia ya Gongo la Mboto, rangi ya dhahabu inawakilisha njia
ya Mbagala, nyekundu inawakaisha njia ya Mbezi ya Kimara, papo
inawakilisha njia ya Boko na nyeupe inawakilisha njia ya Kariakoo.
Vilevile mwisho wa mwezi huu UDA wataanza kwenda nje ya jiji kama
Chalinze, Bagamoyo, Ikwiriri na Msata, lengo ni kutoa huduma kwa
Watanzania wote katika mikoa ya karibu.
Kwa sasa kuna basi 255 zipo barabarani zinafanya kazi ya kubeba
abiria lakini mpaka ikifika mwisho wa mwaka huu kutakuwa na basi 1000,
lakini pia wana karakana za kulaza mabasi hayo zipatazo tano kama,
Mbagala, Gongo la Mboto, Kariakoo, Boko na Mbezi ya Kimara.