BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) YATOA KAULI KUHUSIANA NA KUCHELEWESHWA KWA POSHO YA MAFUNZO KWA VITENDO
Bodi ya mkopo ya Elimu ya Juu nchini Tanzania (HESLB) inashughulikia tatizo la wanafunzi wanaokwenda kwenye mafunzo kwa njia ya vitend...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/08/bodi-ya-mikopo-ya-elimu-ya-juu-heslb.html
Bodi ya
mkopo ya Elimu ya Juu nchini Tanzania (HESLB) inashughulikia tatizo la
wanafunzi wanaokwenda kwenye mafunzo kwa njia ya vitendo ikiwa na baada
ya kulalamikiwa na jumuiya ya wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini
(TAHLISO).
Akizungumza
na East Africa Radio , Mkurungenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Bodi hiyo, Bw. Cosmas Mwaisobwa amesema wanatambua
kuchelewa kwa fedha hizo kwa baadhi ya wanafunzi katika programu tofauti
katika vyuo vikuu nchini ambapo jitihada zinafanywa na Bodi hiyo
kutatua tatizo hilo kwa ili wanafunzi waweze kuendelea na mafunzo yao
kwa vitendo.
Hata
hivyo Bw. Mwaisobwa hakutoa muda kamili ambao tatizo hilo
litashughulikiwa na wanafunzi hao kupatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo
kwa njia ya vitendo.