MWANAUME ATUHUMIWA KUMPA MIMBA MBWA
Bw. Hamis Juma akijitetea kuhusiana na shutuma za mkewe. “Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) a...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/08/mwanaume-atuhumiwa-kumpa-mimba-mbwa.html
Bw. Hamis Juma akijitetea kuhusiana na shutuma za mkewe.
“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.
Kweli
dunia sasa ni vululuvululu! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Cecilia Hamis (pichani), mkazi wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es
Salaam amemlalamikia mumewe aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba
ametembea na mbwa wao mweusi hadi kumpa mimba.Akizungumza na Uwazi
mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema
alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
Mwanamke anayejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis akiwa na mume wake(mtuhumiwa) Hamis Juma.
SIMULIZI YENYEWE
“Nililigundua
hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala,
nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia
ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana
kumwona mume wangu yuko naye amemshikilia (asomaye na afahamu).
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo.
MARA YA PILI
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku
iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka.
Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika
tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza
akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.”
Akaendelea:
“Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na
tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara
nyingi tunawafungia kwenye banda lao.”
AWAELEZA MAJIRANI
Mwanamke
huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza
majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo.
MJUMBE MWENYEWE HUYU HAPA
Akizungumza
na Uwazi, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa
alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri
kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Mbwa anayedaiwa kupewa mimba na Bw. Hamis Juma.
MAJIRANI WAONA ANACHELEWA
Habari
zaidi zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke huyo
anachelewa kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa
taarifa katika Dawati la Jinsia.
Mkuu wa
dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi nyumbani
kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao
kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3
kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
SWALI LA MSINGI
Uwazi
lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na
kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani
hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
Mbwa akicheza na mwenzie.
JE, MUME ANASEMAJE?
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi
sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa
majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela maisha,
halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa yangu
kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
UWAZI LAMUULIZA DAKTARI WA MUHIMBILI
Uwazi
lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo
lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila kama
huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli basi
yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.”