Rais Kikwete atawazwa kuwa chifu msaidizi wa waluguru na chifu kingalu huko kinole, morogoro, apewa jina la Chidukila

  CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katik...

 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.
  CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvika  mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimkabidhi kifimbo maalumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo


 Mke wa Chifu Kingalu akimkabidhi Mama Salma Kikwete shuka katika sherehe hizo
Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akisikiliza maelezo Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Morogoro Injinia Juliana J. Msaghaa akieleza juhudi za upatikanaji wa maji safi na salama wilayani humo wakati wa sherehe hizo.



  Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia pama lake wakati wa sherehe hizo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14 akibadilishana mawazo na Rais Kikwete wakiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera na kushoto ni msaidizi wa Chifu Kingalu

 Mama Salma Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe hizo, akisisitiza umuhimu wa kinamama kujiunga na SACCOS pamoja na kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa wakati muafaka.

Rais Kikwete akiwaaga wananchi wa Kinole baada ya sherehe hizo.
PICHA NA IKULU

Related

OTHER NEWS 8137446267091117531

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item