SABA MBARONI KWA MAUAJI YA WANAWAKE MKOANI ARUSHA

Na Joseph Ngilisho, Arusha JESHI la Polisi Mkoani hapa linawashililiwa watu saba,wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio ya mauaji na un...


Na Joseph Ngilisho, Arusha
JESHI la Polisi Mkoani hapa linawashililiwa watu saba,wanaotuhumiwa kujihusisha na matukio ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha n'a kuwapiga risasi wanawake.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, Kamanda wa jeshi hilo, Liberatus Sabas,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Japhet Lomnyak (25) mkazi wa Sakina,Nehemia Kweka (34) wa Ngaramtoni, Adam Mussa (30) wa Majengo, Tito Loomoni (25) wa Shamsi, Joseph  Loomoni (29) wa Shamsi, Abdallah Magilani (22) mkazi wa Oldadai na Emmanuel Magilani (23) mkazi wa Oldadai.

Alisema watuhumiwa hao wamehusika katika tukio la Agosti 21 mwaka huu, maeneo ya Olasiti ambapo walkiwa na pikipiki aina ya Toyo, walimjeruhi kwa risasi Christen Nickson mkazi wa Olasiti.

Alisema watuhumiwa walifukuza gari aina ya Corolla na baada ya kusimama walimuamuru dereva ambae ni baba wa marehemu wapatie fedha na kupatiwa shilingi 2,000 huku akiwambia fedha nyengine ziko kwenye gari.

Alisema wakati dereva huyo alipoingia garini huku watuhumiwa wakimsubiri ateremke awapatie fedha, aliondoa gari kwa ghafla na majambazi hayo kufyatua risasi zilizomuua mtoto huyo.





Tukio jengine ni la mauaji ya Shamimu Rashidi Yulu (30) yaliyofanyika Agosti 6 mwaka huu majira ya saa 3:30 usiku katika maeneo ya Kwa Iddi ambapo mama huyo alikuwa akielekea nyumbani kwake.


Alipiogwa risasi shingoni na kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Seliani.

Related

TUJUZANE 6624106038909037981

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item