SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA VYETI HALISI UOMBAJI KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA

Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea...

Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi Hiyo Bi. Riziki Abraham.

Serikali imewataka waombaji kazi waliobadilisha majina, waliosoma nje ya Nchi, kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa na vyeti kufuata taratibu pindi wanapoomba kazi secretariati ya ajira.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Riziki alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko toka kwa waombaji wa kazi kuwa secretariati ya Ajira imekuwa na upedeleo kwa kutowaita au kuwazuia kufanya usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi.
Riziki alifafanua kuwa pindi waombaji wanapokabiliwa na hali hiyo hawana budi kutoa tarifaa katika mamlaka husika ili taratibu za kupata vyeti vingine zifanyike na taarifa zao kutumwa Secretariati ya Ajira kwa wakati.
Akizitaja Mamlaka hizo Riziki alisema ni Polisi, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Vikuu (TCU), na Baraza la Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE).
Aidha, Riziki aliongeza kuwa kwa waombaji wenye majina tofauti kwenye vyeti wanapaswa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria na kwakufanya hivyo itasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina na kutambulika kisheria.

Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake, hususani waombaji kazi Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.

Related

SMZ YAZUIA KIWANJA CHA WATOTO KUTUMIKA SIKUKUU ZA IDD EL FITR

Na Rahma Suleiman   Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema kiwanja cha kufurahisha watoto kilichopo eneo la Kariakoo, mjini Unguja, hakitatumika katika Sikukuu ya Idd El Fitr, mwa...

NAPE: DR. SLAA NA UKAWA WAMEKOSA HOJA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Sekretarieti,Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba,ambapo aliwaeleza kuwa Kamati Kuu imemteua&...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item