WANAFUNZI WA STASHAHADA YA UALIMU WA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI UDOM KUNUFAIKA NA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

M kurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waand...

Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.


Frank Mvungi_ Maelezo
Serikali  imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
“ Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya Juu.”Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, Mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .
Aidha Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo  yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi  ambayo ni www.heslb.go.tz .na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa.

Related

MATOKEO YA KIDATO CHA SITSA 2015

Kutazama matokeo ya kidato cha sita - 2015  bofya HAPA.

Late Post: MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT 2015 HAYA HAPA

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA ANA WATANGAZIA VIJANA IDADI 20000 WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2015 KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA. WANATAKIWA KURIPOTI KWENYE VIKOSI VYA MAFUNZO...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item