Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi
Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani)...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/10/bodi-ya-huduma-za-maktaba-tanzania.html
Mkuu wa Kitengo cha Mipango
kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba akiwaeleza
waandishi wa habari(hawapo pichani) Kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na
Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo cha ukutubi na uhifadhi wa
nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa maktaba za wilaya za Kibaha,
Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu, wakati wa Mkutano
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Bi. Georgina Misama.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya
ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo
2014/2015.
Hatua hiyo inatokana na kuongezeka kwa maombi ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo baada ya kuhitimu mafunzo ya cheti.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za
Maktaba Tanzania Bw. Comfort Komba wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam.
Comfort
alisema kuwa masomo hayo kwa awali yalikuwa yakitolewa katika kampasi
ya Bagamoyo lakini kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa masomo hayo
ambapo mpaka sasa kuna wanafunzi wapya 130
“Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania imeamua kuanzisha masomo ya jioni ya
diploma ya ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa
masomo 2014/2015 na utaratibu huu tunautekeleza kutokana na kuwepo kwa
ongezeko la uhitaji wa wanafunzi” Alisema Comfort.
Aidha
Comfort alisema kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kwa
kushirikiana na halmashauri za Wilaya na Mikoa imefanikiwa kuanzisha
maktaba katika wilaya mbalimbali ikiwemo Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara,
Rulenge, Masasi na Mbulu.
Akizungumzia
kuhusu uhufadhi wa machapisho ya kitaifa, Comfort alisema kuwa Ofisi
hiyo imefanikiwa kuhifadhi jumla ya vitabu 1,300,000 pamoja na majarida
950,000 tangu Bodi hiyo ilipoanzishwa katika ngazi ya Mikoa, Wilaya hadi
Tarafa.
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ni Shirika la umma lililopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.