AMAVUMBI KUTUA MWANZA JANUARI 21

KIKOSI CHA AMAVUMBI Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) itawasili Mwanza, Tanzania Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafik...

KIKOSI CHA AMAVUMBI

Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) itawasili Mwanza, Tanzania Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.

Baada ya kocha Mdachi, Mart Nooij kutaja kikosi, Stars inaingia kambini keshokutwa (Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.

Kikosi hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa na wachezaji 26.

 

Related

TUJUZANE 7868955491922524782

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item