JERMAIN DEFOE ATUA SUNDERLAND

 Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza Jermain Colin Defoe amejiunga na timu ya Sunderland. Defoe mwenye miaka 32 ...


 Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza Jermain Colin Defoe amejiunga na timu ya Sunderland.

Defoe mwenye miaka 32 aliekua akiichezea timu ya Toronto FC ya nchi Marekani amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kuweza kuitumikia timu hiyo.

Mshambuliaji huyu mwenye uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu alijiunga na Toronto akitokea klabu ya Tottenham alikocheza kwa mafanikio makubwa .

Alifunga Zaidi ya magoli 120 katika ligi England akiwa anazitumikia timu za West Ham United, Portsmouth and Tottenham Hotspur.

Mshambuliaji Sunderland Jozy Altidore, amepelekwa kwenye timu ya Toronto kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho huo.
BBC Swahili.

Related

TUJUZANE 4743292841556561114

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item