IPTL YASHUSHA BEI YA UMEME KWA ASILIMIA 20
KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa kampuni ya Pan African Power Solution...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2015/01/iptl-yashusha-bei-ya-umeme-kwa-asilimia.html
KAMPUNI
ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa
chini ya uongozi wa kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited
(PAP) imetangaza kufikia kwa punguzo la bei ya umeme la asilimia 20
baada ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo huo ya masaa
36,000 ikifanya kazi, zoezi iliyokamilika ndani ya mwanka 2014.
IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme ikitarajiwa kushuka zaidi kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito.
Marekebisho
hayo yaliyotumia zaidi ya Dola za kimarekani milioni 25 yameiwezesha
mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme wa uhakika
kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika gridi ya Taifa mara to baada
ya kukamilika kwa zoezi hilo mnamo Desemba mwaka 2014.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo,
Bw. Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake
inaoutoza kwa Shirika la ugavi wa umeme Tanzania (Tanesco) ambao sasa
utakuwa chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 dola za
kimarekani kwa Kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa
uhakika.
“Tukiwa
tunaukaribisha mwaka 2015, IPTL inajivunia kutangaza kuwa imefanikiwa
kufanya marekebisho makubwa ya mashine zake ya masaa 36,000 ya kufanya
kazi, zoezi iliyokamilika ndani ya mwaka wa 2014. Nimeiomba timu ya IPTL
kupanga mapema jinsi gani wanaweza kuongeza juhudi zaidi kufikia
marekebisho ya masaa 48,000, katika awamu inayofuata katika mwaka 2015.
Tunatarajia uwepo wa IPTL kuwa bora zaidi kwa kuwa sasa tunajipanga
kuongeza rasilimali zaidi.
“Hii
ni sehemu ya ahadi ya PAP kuhakikisha kuwa IPTL inaendeshwa vizuri na
kwa ufanisi. Wakati sasa umefika kwa TANESCO kuwa na uhakika wa kupata
umeme wa uhakika wa megawati 100 katika gridi ya taifa wakati wowote
utakapohitajika.
“IPTL
chini ya PAP haiangalii tu uzalishaji wa umeme wa kutosha, lakini pia
ipo makini kuhakikisha kuwa umeme huo wa kutosha unakuwa nafuu. Kwa
maana hiyo, tumeamua kushusha bei zetu za umeme kufikia chini ya bei
iliyokokotolewa ya hapo awali ya senti 23 dola za kimarekani kwa uniti,
ambayo sasa inaleta jumla ya punguzo la bei la asilimia 20 kwa ile
iliyokuwa ikitozwa na IPTL kabla ya PAP kuchukua uongozi,” alisema.
Bw.
Sethi aliongeza kuwa TANESCO itarajie punguzo zaidi la bei ya umeme
kufikia kiwango cha chini ya Senti 8 Dola za kimarekani kwa kila uniti
ya umeme mara baada ya mitambo ya IPTL kupanuliwa na kufikia uzalishaji
wa megawati 500 mitambo yake ikitumia gesi asilia.
Alisema
kuwa mpango wa upanuzi wa mitambo hiyo unaendelea vizuri, akiongeza
kuwa iko katika hatua za awali za uchanganuzi na upimaji wa udongo.
“Tunatarajia
hatua za upanuzi kwenda haraka ili kuhakikisha kuwa IPTL inatoa huduma
bora, ya uhakika na nafuu katika taifa hili. Ningependa kutoka shukrani
zangu kwa uongozi wa TANESCO na Gridi ya Taifa kwa kukubali umeme
unaozalishwa na IPTL,”alisema.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbali mbali kutoka TANESCO, bei za umeme zinazotozwa
na IPTL kwa sasa zimeshuka na kufikia chini ya Senti 19 Dola za
kimarekani kwa uniti za umeme kutokana na kushuka kwa bei ya Mafuta
mazito wakati wa kipindi cha ukokotoaji wa bei hizo.
Upatikanaji
wa umeme wa uhakika kutoka IPTL tayari umeshathibitika wakati wa
kipindi cha sikukuu kilichopita ambapo nchi haikukumbana na mgawo wowote
ikilinganishwa na miaka iliyopita ambapo ilikuwa ni kawaida kwa umeme
kukatika katika wakati wa msimu wa sikukuu ambapo kunakuwa na mahitaji
makubwa.