MADIWANI MANISPAA YA MOSHI WASUSIA KIKAO CHA BAJETI
Diwani wa kata ya Kaloleni ,Michael Mwita (CCM) akizungumza juu ya kitendo cha madiwani wenzake kutoka nje huku wakituhumu Mkurugenz...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2015/01/madiwani-manispaa-ya-moshi-wasusia.html
Diwani
wa kata ya Kaloleni ,Michael Mwita (CCM) akizungumza juu ya kitendo cha
madiwani wenzake kutoka nje huku wakituhumu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
kuhusika katika uporaji wa viwanja vya halmashauri hiyo.
Diwani
wa kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akiongozana na mbunge wa jimbo la Moshi
mjini Philemoni Ndesamburo kutoka nje ya ukumbi huo.
Msathiki
Meya akizungumzia msimamo wake juu ya hatua ya wajumbe wa baraza hilo
kutoka nje ya ukumbi wa mikutano wakimtuhumu mkurugenzi wa manispaa hiyo
,Shabani Ntarambe kujihusisha katika uporaji wa Viwanja.
Mkurugenzi Shabani Ntarambe akitoka ukumbini.
Mstahiki
Meya Jafary Michael pamoja na Madiwani wengine wakijaribu kuzungumza
na diwani wa kata ya Kilimanjaro Piscus Tarimo aliyebaki ukumbini wakati
wenzake wakitoka .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MGOGORO
mkubwa umetokea katika kikao cha baraza la Halmashauri ya Manispaa ya
Moshi baada ya Madiwani kususia kikao cha Bajeti ya Manispaa hiyo
kilichokuwa kiketi jana, wakitaka iundwe tume ya kuchunguza madai ya
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Shabani Ntarambe kushiriki katika uporaji
wa moja ya kiwanja zilipo ofisi za kata ya Mawenzi.
Dalili
za kutokea kwa mgomo huo zilionekana mapema baada ya kikao cha baraza
hilo,chenye utaratibu wa kuanza saa 4 :00 kamili kuchelewa kuanza huku
madiwani wakionekana katika viunga vya manispaa hiyo wakiwa katika
makundi tofauti wakiendelea na vikao visivyo rasmi.
Majira
ya saa 4:20 mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akiwa
ameongozana na Naibu Mstahiki Meya Dkt ,Charles Mmbando ,mkurugenzi wa
Manispaa hiyo,Ntarambe waliingia ukumbini na kisha Meya kufungua kwa
sara .
Kabla
ya Mstahiki Meya Kufungua kikao ,ndipo alipo nyoosha mkono ,Diwani wa
kata ya Rau,Peter Kimaro alinyoosha mkono na kuwasilisha hoja kwa niaba
ya madiwani wenzake ya kumtaka Meya asifungue kikao.
“Mh
Mstahiki Meya ,Jukumu na wajibu wa madiwani ni kutetea na kulinda mali
za wananchi vikiwemo viwanja,taarifa sahihi tulizo nazo ni kwamba
mkurugenzi Shabani Ntarambe ameshiriki kupora kiwanja zilipo ofisi za
kata ya Mawenzi.”alianza kusema Kimaro.
Alisema
mkurugenzi huyo ameondoa kwa siri zuio lililowekwa na baraza la
halmashauri kwa msajili wa ardhi kwa lengo la kuzia utolewaji wa hati ya
kiwanja hicho bila ya kumshirikisha mstahiki Meya na baraza la
madiwani.
Kimaro
alisema jambo jingine alilofanya mkurugenzi huyo ni kuagiza wataalamu
wake kutengeneza hati ya umiliki kwa mtu binafsi na kwamba amedharau
agizo la baraza hilo lililotolewa Aprili 17 mwaka jana lililomwagiza
kupata hati ya eneo hilo kwa jina la Halmashauri.
“Kwa
sababu hizo wajumbe wa baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
kupitia Chadema hatuwezi kuendelea na kikao cha baraza mpaka hapo
Mstahiki Meya itakapo undwa tume na kuandaa kikao cha baraza cha
kujadili kadhia hii.” Alisema Kimaro.
Baada
ya Kimaro kumaliza kutoa shutuma hizo ndipo madiwani walisimama
isipokuwa wale wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakitoka nje ya
ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo huku wakiimba na kupiga makofi.
Hata
Mkurugenzi (Ntarambe) alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma dhidi
yake aligoma kuzungumza na waandishi wa habari akidai kuwa na haraka ya
wito katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
“Kwa
sasa hatuwezi zungumza chochote kwa ajili ya muda ,naelekea mkuu wa mkoa
ameiiita kwa sababu ya suala hili hili,mimi nadhani tupeane muda au
muendelee kunisubiri hadi nitoke kwa mkuu wa mkoa takuja
tuzungumze”alisema Ntarambe huku akiondoka ofisini kwake na kuwaacha
waandishi wa habari.