SPLM KUMALIZA MGOGORO SUDAN KUSINI

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  leo tarehe 22/01/2015  kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ...

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  leo tarehe 22/01/2015  kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini,  Mhe Cyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, Rais Salva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji
saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Yoweri Museveni  leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini
makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjane wa Mwenyekiti wa Zamani wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng Garang de  Mabior leo Jumatano kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini,  Mhe Cyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, Rais Salva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar.

PICHA ZOTE NA IKULU

Makundi yanayopingana nchini Sudan Kusini yamekusanyika nchini Tanzania kusaka jitihada mpya za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha maelfu ya watu kuuawa.

Serikali ya Tanzania ambayo inasimamia mazungumzo ya Arusha kupitia chama tawala cha CCM nchini humo, imesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake na sasa kuwa kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar walikutana Jumatano na kutiliana saini mkataba mpya wa amani.

Pande mbili hizo zilitiliana saini mkataba unaolenga kukiunganisha chama tawala cha the Sudan People's Liberation Movement (SPLM), ili kumaliza uhasama uliojitokeza miongoni mwa viongozi wa chama hicho kilichopigania uhuru wa Sudan Kusini miaka mitatu iliyopita.

Vita vilizuka nchini Sudan Kusini, taifa changa kuliko yote duniani, mwezi Desemba 2013 wakati Kiir alipomshutumu naibu aliyemfukuza Machar kwa jaribio la kumpindua.

Mara ya mwisho Kiir na Machar walikutana mwezi Novemba, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako walikubaliana kusitisha haraka vita, mkataba uliovunjwa katika muda wa saa chahche tangu wakubaliane.

Mapigano katika mji mkuu wa Juba yamesababisha mauaji ya kulipiza kisasi nchini humo na kuisukuma nchi kuingia katika kipindi cha njaa.

Shughuli za kutiliana saini mkataba wa amani kati ya Rais Kiir na Bwana Machar zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kikanda kushuhudia mkataba wa umoja kw makundi tofauti ya chama tawala cha SPLM.

Mazungumzo ya Tanzania yanafanyika sambamba na juhudi za kuleta amani zilizokuwa zikisimamiwa na nchi za IGAD mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Awamu nyingine ya mazungumzo ya IGAD yanatarajiwa kufanyika kando ya kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa mwishoni mwa Januari.
Lakini vita vinaendelea.

Wiki hii msemaji wa jeshi Philip Aguer amesema jeshi na waasi wamekuwa na mapigano makali katika jimbo la Central Lakes, na ameshutumu majeshi ya Machar kwa kulipua kisima cha mafuta katika jimbo la Unity.

"Majeshi ya Machar yamekuwa yakisababisha uharibifu, uchomaji wa vijiji, uharibifu wa visima vya mafuta," amesema.
Ni mara ya kwanza waasi mahasimu hao kukutana tangu waliposaini makubaliano ya kuacha mapigano mwezi Agosti huko Ethiopia, ambayo kama mikataba mitatu iliyopita ilivunjika mara moja.

Viongozi hao wa siasa na kijeshi wamekuwa wakirudia rudia kuvunja ahadi wanazotoa chini ya msukumo wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Sudani ya Kusini uliofanywa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Waziri Mkuu wa Marekani John Kerry.
Safari hii viongozi hao wawili wa Sudani ya Kusini walisema chama tawala kilichogawanyika, Sudan People's Liberation Movement (SPLM), inapaswa kuungana upya. Chama cha SPLM kiliiletea nchi uhuru baada ya vita vya muda mrefu na Khartoum.

"Chama kilichogawanyika cha SPLM kitaigawa nchi katika makundi ya kikabila na maeneo," makubaliano hayo yalieleza, kutoa wito kwa "mazungumzo ya halali na ya uaminifu ambayo yanaweka matakwa ya watu na taifa juu ya wote".
Kiir alitoa ahadi ya "utatuzi kwa amani wa mgogoro" katika nchi iliyokuwa maskini wakati ina utajiri wa mafuta, ambayo ina miaka mitatu lakini iliyokumbwa na vita.
"Hakuna sababu kwa watu wetu kupata shida tena baada ya uhuru," alisema. Machar pia alisema alitaka jambo hilo kumalizika.

"Hatutaki fursa hii kutoweka kama fursa nyingine za awali," alisema. "Tutafanya kwa uwezo wetu wote kuona kuwa mchakato huu unamalizika"
Kikundi cha tatu kilichojitenga katika SPLM -- viongozi wa ngazi ya juu walifungwa kwa miezi kadhaa baada ya vita kuibuka mwezi Desemba, lakini pia walisaini suala hilo la kuunganisha chama.

Related

OTHER NEWS 7116579253265331169

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item