MKE WA RAIS WA UJERUMANI BI DANIELA SCHADT MGENI RASMI UFUNGUZI WA SKULI MWERA

Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt.akiondoa kipazia kuashiria ufunguzi wa Skuli hiyo huko Mwera Wilaya ya Kati Unguja. ...

Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt.akiondoa kipazia kuashiria ufunguzi wa Skuli hiyo huko Mwera Wilaya ya Kati Unguja.

 Jengo la Skuli ya Herrnhuter Academy School, ilioko katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Kati Unguja, iliofunguliwa na Mke wa Rais wa Ujerumani wakati wa ziara yake Zanzibar.

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana na Wanawake Zanzibar Mhe Zainab Omar Mohammed, wakiwasili katika viwanja vya Skuli ya Herrnhuter Academy School, ilioko Mwera Wilaya ya Kati Unguja, kwa ajili ya ufunguzi wa skuli hiyo.

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akifungwa Ua na wanafunzi wa Skuli hiyo baada ya kuwasili katika hafla ya ufunguzi wa majengo ya Skuli hiyo mwera Zanzibar

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akiongea na Viongozi wa Kanisa la Monrovia Zanzibar baada ya kuwasili katika viwanja vya Skuli hiyo kwa ajili ya ufunguzi wake. alipofika Zanzibar kwa ziara ya siku moja na Mumewe Rais wa Ujerumani.

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akisalimiana na Viongozi wa Kanisa la Monrovia inayomiliki Skuli hiyo, alipowasili katika viwanja vya skuli hiyo kwa ajili ya ufunguza wa skuli hiyo mwera.  

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akipokelewa na Wazazi na Viongozi wa Skuli hiyo alipowasili katika viwanja vya Skuli Mwera.

 Wanafunzi wa skuli hiyo wakimpokea Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, alipofika skulini hapo kuwafungulia Skuli yao wakati alipofika Zanzibar kwa ziara ya siku moja na Mumewe Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck

 Mkuu wa Wilaya ya Kati Mhe Ayoub Mahmaud, akizungumza wakati wa hafla hiyo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdallah Mwinyi. wakati wa hafla ufunguzi wa skuli hiyo 

 Viongozi wa Kamati ya Skuli na Wazee wa Wanafunzi wanaosoma skuli hiyo wakifuatilia ufunguzi huo wakiwa katika viwanja vya skuli mwera.

 Wanafunzi wa Skuli hiyo wakipeperusha bendera ya Ujerumani wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa skuli hiyo mwera. 

 Wanafunzi wa Skuli ya hiyo wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt.wakati wa ufunguzi huo.

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt.akiwahutubia Wanafunzi na Wazee wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli hiyo, hafla hiyo imefanyika katika majengo yake mwera Zanzibar. 

 Mkuu wa Skuli ya Herrnhuter Academy School, historia ya Ujenzi wake kabla ya ufunguzi uliofanya na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt.

 MKE wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akikata utepe kuashiria kuifungua ya Skuli ya Maandalizi ya Herrnhuter Academy School iliko  Mwera Wilaya ya Kati Unguja,Bi Daniela akiwa Zanzibar na Mumewe Rais wa Ujerumani kwa ziara ya siku moja Zanzibar.

 Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt. akikabidhi vifaa vya michezo na vitu vya kuchezea kwa wanafunzi wa skuli hiyo


 MKE wa Rais wa Ujerumani akipokea zawadi ya Visiwavya Unguja na Pemba na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Monrovia Zanzibar Hoseya Siwelwe, wakati wa hafla ya uzinduzi wa skuli hiyo ilioko mwera Zanzibar.


 MKE wa Rais wa Ujerumani Bi Daniel Schadt, akiwauliza maswali wanafunzi wa skuli hiyo baada ya uzinduzi wa majengo ya skuli yao ilioko mwera Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja

Related

OTHER NEWS 8405540948682967406

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item