Askari Polisi aliyeuliwa kikatili Mkoani Dodoma aagwa , Muuaji naye auliwa na wananchi

  Jeneza liliobeba mwili wa marehemu likiwa mbele ya waombolezaji  wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa jana tarehe 05...

 Jeneza liliobeba mwili wa marehemu likiwa mbele ya waombolezaji  wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa jana tarehe 05/02/2015.


 Wasifu wa marehemu ukisomwa 

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu akiongoza  waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Askari Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI aliyeuwawa huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI SIRIL MALYA.


Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma. 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi Askari huyo.
Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua Askari. 
Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. 
Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua. 
Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi. 
Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

Related

YANGA YAFUZU VPL

Yanga imefanikiwa kuifunga Komorozine bao 5-2 hivyo kufuzu kuvuka raundi ya kwanza ya mashindano haya ya CAF, katika mchezo huu Ngassa aliifungia timu yake mabao 3.

TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ndugu wanahabari na wa Tanzania wenzangu, Nimekuwa nikilazimika kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki kuhusiana na namna mchakato wa kuandika katiba mpya y...

GRACE MVANDA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA IRINGA

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha Grace Tendeya Mvanda, kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo la Kalenga, mkoani Iringa. Grace M...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904822

HOT POSTSRECENTArchive

RECENT

Archive

item