NAFASI ZA KAZI: TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA, DEADLINE 16/02/2015

AJIRA - TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA - 2/2/2015 1.0 Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa mujibu wa aya ya 112 (1) ...



AJIRA - TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA - 2/2/2015
1.0 Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilicho undwa kwa mujibu wa aya ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Aidha kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine, inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

1.1 Hivyo tume ya utumishi wa mahakama inawatangazia watanzania wenye sifa zilizo ainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wapo tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania ambazo zipo katika mikoa na wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.

2.0 Afisa utumishi II (TGS D) - Nafasi 80.
2.1 Sifa:
             Shahada ya kwanza ya sayansi ya jamii au sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyo tambulika na serikali ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
- Menejimenti ya rasilimali watu (Human resource management)
- Elimu ya jamii (Sociology)                                                        
- Utawala na Uongozi (Public Administration)                          
- Mipango ya watumishi (Manpower planning)                        
- Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.                                    
2.2 Waombajin watapangiwa kazi Mahakama za wilaya isipokuwa za mkoa wa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe wilaya tatu (3) zilizopo katika mojawapo ya mikoa ifuatayo: Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Shinyanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza lisizingatiwe. Aidha, baadaye watabadilishwa kazi kuwa watendaji wa Mahakama.
2.3 Kazi za Afisa utumishi Daraja la II
(i) Kutunza kumbukumbu sahihi za watumishi wote.
(ii) Kutafsiri na kushughulikia miundo ya utumishi.
(iii) Kutafiti, kuchanganua, kupanga, na kukadiria idadi ya watumishi wanao hitaji mafunzo.
(iv) Kukusanya, kuchambua, na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
(v) Kushughulikia masuala mbalimbali ya kila siku ya watumishi.
(vi) Kusimamia OPRAS


3.0 Afisa Tawala II - TGS D - Nafasi 80
3.1 Sifa
Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyo tambuliwa na serikali katika fani zifuatazo:-
Utawala, Elimu ya jamii, Sheria (Mwenye cheti cha Law school), Menejimenti ya Umma, Uchumi na wenye ujuzi wa kompyuta.
3.2 Waombaji watapangiwa kazi katika mahakama za Wilaya isipokuwa za mkoa wa Dar es Salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe wilaya tatu (3) zilizopo katika mojawapo ya mikoa ifuatayo:- Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Shinyanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza lisizingatiwe. Aidha, baadaye watabadilishwa kazi kuwa Watendaji wa Mahakama.

1.3 Kazi za Maafisa Tawala
(i) Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu.
(ii) Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na taratibu mbalimbali.
(iii) Kusimamia kazi za Utawala na Utendaji.

4.0 Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani (Internal Auditor) Daraja la II TGS D - Nafasi 25
4.1 Sifa
(i) Wenye Intermediate Certificate inayo tolewa na NBAA.
(ii) Wenye shahada ya Biashara au Sanaa yenye mwelekeo wa uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu (UDA) kutoka Chuo au Taasisi yoyote inayo tambuliwa na Serikali.
(iii) Wenye Stashahada ya juu katika Uhasibu wa Serikali (Advanced diploma in Government Accounting) kutoka chuo cha uhasibu Dar es salaam (DSA)
4.2 Waombaji watapangiwa kazi Mahakama Kuu - Kanda au Ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi isipokuwa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe Kanda/Mikoa mitatu (3) kati ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Shinyanga ambayo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao laweza lisizingatiwe.
4.3 Kazi za Mkaguzi wa Hesabu za Ndani Daraja la II
(i) Kufanya ukaguzi wa Hesabu.
(ii) Kusahihisha na kuidhinisha ripoti ya Ukaguzi.
(iii) Kusahihisha na kuidhinisha hoja za ukaguzi wa ndani ( Internal Audit queries)

5.0 Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja la II - TGS D - Nafasi 15.
5.1 Sifa
Shahada/Stashahada ya Juu katika masomo ya Sayansi ya Kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinacho tambuliwa na Serikali.
5.2 Waombaji watapangiwa kazi Mahakama Kuu - Kanda isipokuwa Dar es salaam. Waombaji wa nafasi hii waonyeshe kanda tatu (3) kati ya zifuatazo: Arusha, Bukoba, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mwanza, Mtwara, Songea, Sumbawanga, Tabora na Tanga ambazo wangependa kupangiwa ingawa pendekezo lao linaweza lisizingatiwe.
5.3 Kazi za Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Daraja II
(i) Kuweka kumbukumbu za taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi.
(ii) Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na udhibiti unaohusu Kompyuta.
(iii) Kutoa msaada wa kiufundi kwa Wizara/Idara/Vituo mbalimbali vya kazi.

6.0 Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 16/02/2015 saa 9:30 Alasiri.

7.0 Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatanisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV)
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Waombaji walio katika utumishi wa Umma wanapaswa kupitisha maombi yao kwa waajiri wao na walio wahi kuacha kazi katika utumishi wa Umma waeleze bayana kuwa waliacha kazi katika utumishi wa Umma.

Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P 8391, DAR ES SALAAM.

Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.

Related

KAZI 7453573625351570023

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item