MAGUFULI: NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

MGOMBEA urais kwa teketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi...

MGOMBEA urais kwa teketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.

Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.
Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo  katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Korogwe, Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini 


  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe mjini  Mary Chatanda Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya chuo cha ualimu Korogwe.

 Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa,Ndugu Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani humo.

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bumbuli kwenye viwanja vya Togotwe ambapo aliwaahidi kuwajengea barabara ya lami pamoja na kufuatilia suala la kiwanda cha Chai cha Mponde.


 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo.





Wananchi wa Lushoto mjini wakishangilia jambo mara baada ya kumsikia Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia .

Related

SOMA UJUMBE WA KWENYE BANGO UNAOMUHUSU LOWASA ALIOPOKELEWA NAO SUMAYE ALIPOINGIA MWANZA

 Hapa ni baadhi ya washiriki kwenye kongamano lilofanyika katika ukumbi wa nyanza jijini mwanza, washiriki walikuwa wanafunzi wa vyuo jijini mwanza  Wakifatilia........... &nbs...

MBUNGE WA CCM JIMBO LA BAHI AKUMBWA NA KASHFA NZITO KATIKA MFUKO WA JIMBO MKOANI DODOMA

DODOMA.  MBUNGE wa Bahi (CCM), Omar Badwel ameingia katika kashfa baada ya Kamati ya Uhakiki wa Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kubaini matumizi mabaya ya fedha hizo. Kamati hiyo il...

KATIBU MKUU WA UN AONYA KUHUSU GHASIA AFRIKA YA KATI (CAR)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ameonya kuwa ghasia zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, zinaweza kuligawa taifa hilo na kuwatenga kabisa Wakristo na Waislamu. Bwana B...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904820
item