AHUKUMIWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA NA KUMZALISHA MWANAYE

Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe akiwa kizimbani. Yusufu akificha sura ya...

Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe akiwa kizimbani.
Yusufu akificha sura yake asipigwe picha baada ya hukumu ya miaka 30.

Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakati wakitoka mahakamani. Kushoto ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa.

 MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.

Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa miaka minne hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.

Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa  Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.

Aidha kabla ya kutoa hukumu, Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.

Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo, Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “mfa maji haachi kutapatapa”

HABARI NA MBEYA YETU BLOG

Related

TASWIRA: RAIS KIKWETE ALIPOWASILI ABUJA, NIGERIA KUHUDHURIA MKUTANO WA UCHUMI DUNIANI

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudh...

TAARIFA YA JESHI LA POLISI BOMU LILOLIPUKA MWANZA

Usiku wa May 5 2014 yani jana saa mbili na dakika 20 umetokea mlipuko mwingine ndani ya kanisa la KKKT Makongoro wilayani Ilemela Mwanza  ambao umethibitishwa na Polisi.olisi imethibitis...

TAARIFA ZA JESHI LA POLISI KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA DODOMA

Kutoka Dodoma Mei 05 majira ya saa saba mchana kulitokea vurugu zilizoanzishwa na wabeba mizigo wa Mji mdogo wa Kibaigwa ambapo taarifa inasema zilikua ni vurugu zilizosababisha magari kadhaa ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item