CUF: NDUNGAI ANAHUJUMU
Chama cha Wananchi (Cuf), kimesema kitendo cha Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kukataa kumpa nafasi Kiongozi wa Kambi ya Upin...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/09/cuf-ndungai-anahujumu.html
Chama
cha Wananchi (Cuf), kimesema kitendo cha Naibu Spika wa Bunge, Job
Ndugai kukataa kumpa nafasi Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe na kuamuru askari wa Bunge wamtoe nje ya ukumbi huo ni
kumhujumu Rais Kikwete kwenye azma yake ya kupata Katiba Mpya.
Pia,
chama hicho kimesema kinafanya juhudi za kuwasiliana na viongozi wa
vyama vingine ili kuweka mkakati wa pamoja wa kukabiliana na hujuma
dhidi ya mchakato wa kupata Katiba Mpya na kuimarisha umoja wa kitaifa
kwenye kipindi hiki cha kukabiliana na changamoto za nchi jirani.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba
alisema, Cuf inalaani vitendo vya kuwanyanyasa na kuwadhalilisha
wabunge wa upinzani akiwamo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
na kudai kuwa inaonyesha wazi CCM wanampango wa kutengeneza katiba ya
upande mmoja.
“Kwa
mfumo wa mabunge ya Jumuiya ya Madola, kwa Tanzania Waziri Mkuu na
kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ndiyo wanawakilisha pande
mbili ndani ya Bunge, hivyo kumnyima Mbowe fursa ya kuzungumza ni
unyanyasaji na udhalilishaji na kwamba kitendo hicho hakikubaliki,”
alisema.
Profesa
Lipumba alisisitiza muswada uliokuwa unajadiliwa ulikuwa na utata,
Serikali imeubadili kwa nguvu na kuondoa maoni muhimu ya wadau.