WAJUA KWA NINI UNAHITAJI KULALA?
Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi. Wanasema kuwa kulala...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/09/wajua-kwa-nini-unahitaji-kulala.html
Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi.
Wanasema kuwa kulala kunasaidia katika kujenga celi mpya za ubongo.
Usingizi unasaidia kuzalisha upya
celi za ubongo ambazo nazo hujenga kemikali inayojulikana kama Myelin
ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi.
Matokeo ya utafiti huu ambayo yalijitokeza
katika panya wa mahabara, huenda yakachochea maelezo zaidi kuhusu
umuhimu wa usingizi katika kukabarabati celi za ubongo na kukuza celi
mpya pamoja na kuulinda kutokana na magonjwa.
Daktari Chiara Cirelli na wenzake kutoka chuo
kikuu cha Wisconsin waligundua kuwa Panya hao walipokuwa wanalala, ndipo
kemilaki hiyo ilikuwa inatengezwa kwa wingi na celi za mwili.
Ongezeko la kemikali pia ilitegemea aina ya usingizi ambao Panya walilala hasa uliohusishwa na ndoto.
Kinyume na hili, celi zilionekana kufariki wakati Panya walipokuwa wako macho wazi
Na hii ndio maana usingizi ni muhimu jambo
ambalo wamekuwa wakilihoji wanasayansi kwa miaka mingi. Yaani nini
umuhimu wa usingizi?
Ni wazi kuwa tunahitaji kulala ili kupumzika na
ili ubongo wetu ufanye kazi vyema....lakini mambo ya kibayolojia
yanayofanyika tunapokuwa tumelala ndio yameanza tu kugunduliwa.
Daktari Cirelli alisema kuwa : "kwa muda mrefu,
watafiti wa usingizi wamekuwa wakilenga tofauti iliyopo kati ya celi za
neva wakati wanyama wanakuwa hawajalala na wakti wamelala. Kwa sasa ni
bayana kuwa celi zengine kwenye mfumo wa neva hubadilika kutokana na
usingizi.''
Watafiti hao wanasema kuwa matokeo yao
yanapendekeza kuwa ukosefu wa usingizi,unaweza kusababisha maradhi ya
ubongo yanayoathiri celi zake.
Watafiti hao pia wanataka kuchunguza ikiwa
vijana kukosa usingizi wakati wanapokuwa huenda ikaathiri ubongo wao
katika siku za usoni.
Usingizi ni muhimu kwa mfumo wa neva mwilini ili uweze kufanya kazi vyema.
Usingizi pia husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazowafanya watoto na vijana kukuwa.
SOURCE: BBC