WANANDOA WASHAURIWA KUTATUA MATATIZO YAO KWA MAZUNGUMZO; SOMA TAARIFA HII KUTOKA MKOANI MBEYA
“PRESS RELEASE” TAREHE 22. 11. 2013 . WILAYA YA MBARALI – MAUAJI. MNAMO TAREHE 21.11.2013 MAJIRA YA SAA 07:00HRS HUKO KATI...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/11/wanandoa-washauriwa-kutatua-matatizo.html
“PRESS RELEASE” TAREHE 22. 11. 2013.
WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 21.11.2013 MAJIRA YA SAA 07:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MAHANGO, KATA YA MADIBILA , TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA
WA MBEYA. JITIHADA D/O MAMGA, MIAKA 20, MBENA, MKULIMA, MKAZI WA
MAHANGO ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIWA NYUMBANI NA MUME WAKE GERVAS
S/O KADAGA, MIAKA 25, MSANGU, MKULIMA, MKAZI WA MAHANGO. MWILI WA
MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA TISA YA KUCHOMWA KISU SEHEMU MBALIMBALI.
AIDHA MTUHUMIWA ALIJERUHIWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI NA MAREHEMU NA
AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA
NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA NA KULETA
MADHARA KWA FAMILIA.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 21.11.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
LUBANDA, KATA YA ILIMA, TARAFA YA PAKATI, BARABARA YA
TUKUYU/KYELA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA, GARI T.291 BFZ AINA YA
TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIA
S/O MAPANDE, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU LAINA D/O MWANKINA, MIAKA
53, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJJI CHA LUBANDA NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA KUTELEKEZA
GARI ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA AJALI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA RAIA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Signed by,
[DIWANI ATHUMANI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.