MTANZANIA JACK CLIFF AKAMATWA NA MADAWWA YA KULEVYA HUKO MACAU

Jackie akiwa amewekwa mbele ya waandishi wa habari na mzigo wake wote aliokuwa ameumeza..... Waandishi wa habari wakifanya yao ...

Jackie akiwa amewekwa mbele ya waandishi wa habari na mzigo wake wote aliokuwa ameumeza.....

Waandishi wa habari wakifanya yao


Madawa aliyokuwa amemeza Jack
Jack Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya
Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena kwa Mtanzania mwingineakisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea Macao nchini China jumanne iliyopita.

Mtanzania huyo ni msichana ana jumla ya umri wa miaka 28 aitwae Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China. 

Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani
137,72.

Msichana huyu aliliambia Jeshi la Polisi nchini China kwamba alikua akisafiri kuelekea Guangzhou ambao ni mji ulio chini ya jimbo la Guangdong huko China,Inasemekana Msichana huyu amewahi kushiriki video mbalimbali ikiwa ni pamoja na video ya Nataka kulewa ya Diamond.
Hii ni picha imepigwa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Macao.


Source: Masai

Related

OTHER NEWS 5864118351987535410

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item