RAGE NI MWENYEKITI HALALI WA KLABU YA SIMBA
Ismail Aden Rage ndiye Mwenyekiti halali wa Simba ambapo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtaka kuitisha Mkutano Mkuu kwa muji...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/12/rage-ni-mwenyekiti-halali-wa-klabu-ya.html
Ismail Aden Rage ndiye Mwenyekiti halali wa Simba ambapo Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtaka kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu
wa taratibu za klabu ya Simba.
Kamati imebaini upungufu kadhaa wa kisheria kwenye uamuzi wa Kamati
ya Utendaji ya Simba uliofanywa Novemba 18, 2013 kwa kumsimamisha
Mwenyekiti wao. Upungufu huo ni pamoja na ukiukwaji wa Ibara ya 33 ya
Katiba ya Simba juu uitishaji wa mkutano, ajenda ya kumsimamisha
Mwenyekiti kuwasilishwa kwenye kikao kwa utaratibu wa mengineyo.
Changamoto nyingi zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti huyo zingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Simba.
Hivyo, agizo za Rais wa TFF, Jamal Malinzi kumtaka Mwenyekiti wa Simba aitishe mkutano lipo palepale. Pia Mwenyekiti ametakiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kuzingatia Katiba ya klabu hiyo.
Katika mkutano huo wa kujaza nafasi, ndiyo utakaojadili mgogoro kati
ya Mwenyekiti na Kamati yake ya Utendaji. Nafasi hiyo kwa sasa
inakaimiwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Joseph
Itang’are baada ya Geofrey Nyange aliyekuwa akiishikilia kujiuzulu.