MFANYABIASHARA WA KIKE APIGWA RISASI USONI NA KUPORWA MABEGI MAWILI YA FEDHA KARIAKOO.
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA Mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa kwenye gari mara baada ya kupigwa risasi na majambazi (majira ya saa 12 ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/mfanyabiashara-wa-kike-apigwa-risasi.html
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA
Mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa kwenye gari mara baada ya kupigwa risasi na majambazi (majira ya saa 12 Kasoro jana jioni)
Damu
ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya
kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na
kutoweka.
Askari wakiliondoa gari la mfanya biashara huyo katika eneo la tukio
Raia wakishangaa mwili wa mfayabiashara huo ukiondolowa na polisi
Sehemu ya fremu inayosemekana kuwa ni Duka la mfanyabiashara aliyepigwa Risasi Leo majira ya saa 12 jioni
Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia
ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jana jioni )kwa kupigwa
risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi
mawili yaliyoojaa fedha.
Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho
kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya
mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja
alikuwa na bunduki aina ya SMG.
Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo
hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara
huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine
ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya
Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki
na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha
kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya
biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.
'Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa
risasi na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi
kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha mlio wa pili wa risasi
ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na baada ya
hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile
begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga
maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"
Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi
wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake
wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha
kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma
za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card
kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la
Kariakoo.