ZITTO ATENGWA NA CHADEMA
Mkurugenzi wa Mawasiliano Habari na Uenezi, CHADEMA, John Mnyika Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kukubali pingamizi la ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/zitto-atengwa-na-chadema.html
Mkurugenzi wa Mawasiliano Habari na Uenezi, CHADEMA, John Mnyika |
Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kukubali pingamizi la
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuizuia Kamati Kuu (CC) ya
CHADEMA isimjadili hadi kesi yake ya msingi itakapokuwa imesikilizwa,
chama hicho kimemfungia rasmi kushirikiana na wabunge wenzake katika
shughuli za kisiasa.
Sambamba
na hilo, chama hicho kimesema kuwa kuanzia sasa kinasahau mjadala
kuhusu Mbunge huyo wa Kigoma na badala yake kinajikita kuchapa kazi kwa
ajili ya malengo waliyojiwekea mwaka huu 2014.
Shughuli
ambazo Zitto amefungiwa nazo ni pamoja na zile za nje na ndani ya Bunge
la Jamhuri ya Muungano, hususani zinazohusu kambi rasmi ya upinzani
bungeni, inayoongozwa na CHADEMA.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Habari na Uenezi,
CHADEMA, John Mnyika, alisema uamuzi wa mahakama haujaelekeza kwamba
Zitto apewe ushirikiano na chama chake, hivyo uamuzi wa CC wa
kutoshirikiana naye uko pale pale.
Katika uamuzi wa CC uliosomwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, pamoja na kutangaza uamuzi wa kuwavua uanachama Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo, alisema: “Kwa vile Zitto Zuberi Kabwe amekishitaki chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama na kanuni zake, na kwa vile Mahakama Kuu imeamuru vikao vyote vya chama visijadili wala kuamua suala lolote linalohusu uanachama wa Zitto, viongozi wa ngazi zote za chama wanachama, washabiki na wapenzi wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya Tanzania, wasishiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yoyote ya nje au ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto na mawakala wake kwa jina la CHADEMA.”
Katika uamuzi wa CC uliosomwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, pamoja na kutangaza uamuzi wa kuwavua uanachama Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo, alisema: “Kwa vile Zitto Zuberi Kabwe amekishitaki chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama na kanuni zake, na kwa vile Mahakama Kuu imeamuru vikao vyote vya chama visijadili wala kuamua suala lolote linalohusu uanachama wa Zitto, viongozi wa ngazi zote za chama wanachama, washabiki na wapenzi wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya Tanzania, wasishiriki wala kusaidia kwa namna yoyote mikutano yoyote ya nje au ndani au shughuli nyingine yoyote ya kisiasa itakayofanywa na Zitto na mawakala wake kwa jina la CHADEMA.”
Mnyika
alisema Kamati Kuu ilishapitisha azimio la kumtenga Zitto na shughuli
za siasa na kuwataka wanachama wao kote nchini, wasitoe ushirikiano kwa
kazi au shughuli yoyote itakayofanywa na mbunge huyo.
“Uamuzi
huo upo pale pale, na mahakama haijaelekeza kwamba apewe ushirikiano,”
alisema Mnyika wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.
Mnyika
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, aliwataka wafuasi wa CHADEMA kutambua
kuwa kilichoamriwa na mahakama ni pingamizi la awali tu kwani kesi ya
msingi bado haijaanza kusikilizwa.
“Unajua
kilichoamriwa ni pingamizi la awali. Huko ni sawa na kushangilia bao
wakati mpira ndio kwanza umeanza na unaendelea. Mfano mzuri ni kwenye
mechi ya Ligi Kuu ya Simba na Yanga. Yanga walishangilia mabao matatu ya
kipindi cha kwanza wakijua wameshinda, walipoingia kipindi cha pili
unajua kilichotokea… Kwa hiyo kesi ya msingi bado, na hatuoni sababu ya
kushangilia kwa sasa,” alisema.
Mnyika
aliwataka wanachama wao kutambua kuwa CHADEMA iko imara na inaendelea
na kazi zake kama kawaida, huku ikiwa na ajenda muhimu na mikakati
mizito kwa ajili ya mwaka 2014.
Alizitaja
baadhi ya ajenda ambazo wananchi wataanza kuzifanyia kazi kuwa ni
pamoja na suala la katiba ambapo chama hicho kimepitisha maazimio sita
mazito ya kuyafanyia kazi kuelekea mchakato wa katiba mpya na maandalizi
ya mpango kazi wa mwaka 2014.
“Kamati
Kuu iliyopita, mbali ya kushughulikia suala la wanachama wetu wasaliti,
pia ilikuwa na mambo mengi ya kujadili. Kuna maazimio sita ya mchakato
wa katiba mpya ambayo tutawaeleza, kuna suala la kupanda kwa bei ya
umeme na maazimio yake. Watanzania wasubiri waone CHADEMA imeazimia nini
katika suala la kupanda kwa gharama za umeme ambapo wameanza kuumizwa
na ongezeko hilo,” alisema Mnyika.
Kwa
msimamo huo wa kumfungia rasmi Zitto kushiriki shughuli za chama, ni
wazi kuwa unazidi kumuweka njia panda Zitto ambaye sasa atabaki kuwa
mwanachama kwa nguvu ya mahakama hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.
Sasa
Zitto ataungana na wabunge wenzake wawili, David Kafulila wa Kigoma
Kusini (NCCR-Mageuzi) na Hamad Rashid Mohammed wa Wawi (CUF) ambao pia
ubunge wao upo kwa nguvu ya mahakama.
Zitto
alifungua kesi Mahakama Kuu siku moja kabla ya CC kuanza vikao vyake
ambavyo vilikuwa vijadili utetezi wa tuhuma zake za kuendesha mkakati wa
siri wa kusaliti chama, akiomba mahakama izuie suala la uanachama wake
lisijadiliwe hadi kesi yake isikilizwe.
Akitoa
uamuzi wa awali, Jaji John Utamwa, alisema kuwa mahakama imeridhia ombi
la Zitto kuwa CHADEMA au chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi
kesi ya msingi itakapomalizika.
Katika
kesi ya msingi, Zitto anaiomba mahakama ikizuie chama hicho kumchukulia
hatua, ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.
Zitto
aliwasilisha maombi dhidi ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA pamoja na
Katibu Mkuu wa chama, Dk. Slaa, akiiomba mahakama itoe zuio la muda kwa
Kamati Kuu kutojadili uanachama wake.
Katika
kesi hiyo, Zitto ameiomba mahakama iizuie Kamati Kuu kujadili uanachama
wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama na kuomba
mahakama imwamuru Dk. Slaa ampe nakala za taarifa za vikao vilivyomvua
uongozi ili akate rufaa.
Katika hatua nyingine, Janeth Josiah anaripoti kuwa CHADEMA
imemtaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna
Suleiman Kova, kuacha propaganda za kisiasa na badala yake awakamate na
kuwachukulia hatua za kisheria, waliohusika kumteka, kumtesa na
kumuumiza mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Temeke, Josephat Yona.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu wa CHADEMA, Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Henry Kilewo, alisema kama Kamanda Kova amechoka kuwa mtumishi
ndani ya jeshi hilo na kufanya siasa, atoke hadharani na kujitangaza.
“Tunamtaka
Kamanda Kova atoke hadharani atangaze kuwa anatumikia chama gani cha
siasa ili tukutane kwenye majukwaa ya siasa na siyo kwenye vyombo vyetu
vya ulinzi na usalama,” alisema Kilewo.
Alisema
polisi inapaswa kuyachukulia kwa uzito mkubwa na unaostahili matukio ya
namna hii ambayo yanaanza kuota mzizi kwenye jamii.
Kilewo
alisema mwaka 2012/2013 yalitokea matukio yenye sura ya aina hiyo ya
kutekwa na kuteswa kwa watu mbalimbali, wakiwamo wanaharakati,
wanahabari na wanasiasa, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa.
Alitoa
mfano kuwa Jeshi la Polisi walimkamata kijana Evodius Justinian na
wenzake, waliwatesa vikali na kuwarubuni katika jitihada za
kuwashinikiza wakiri kuwa viongozi wa CHADEMA ndio waliowatuma
kutekeleza matukio ya uhalifu.
Alisema
bado Watanzania wanataka kujua taarifa na hatua zilizochuliwa kisheria
katika matukio ya kutekwa na kuteswa kwa Dk. Steven Ulimboka na
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Hata
hivyo, alisema CHADEMA ipo mstari wa mbele kutetea haki za binadamu,
kupinga ukatili, uhuni na vitendo kama hivyo na hakiwezi kumtuma mtu
yeyote kufanya utekaji, utesaji au udhalilishaji.
Kwa
mujibu wa Kova, uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa tukio la kutekwa kwa
kiongozi huyo wa CHADEMA, lina uhusiano na ugomvi unaoendelea ndani ya
chama hicho, hivyo ameunda tume ya wataalamu kuchunguza.
Yona alikutwa usiku wa juzi akiwa katika hali mbaya ya kujeruhiwa huko Ununio wilayani Kinondoni.
Source: Tanzania Daima