UJUMBE WA UM COTE D'LVOIRE WAONGEZEWA MWAKA MMOJA ZAIDI
Baraza la Usalama limepitisha azimio leo mjini New York la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire, UNOC...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/ujumbe-wa-um-cote-dlvoire-waongezewa.html
Baraza la Usalama limepitisha azimio leo mjini New York la kuongeza
muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire, UNOCI, kwa
kipindi cha mwaka moja.
Rais wa Baraza hilo Vitaly Churkin akitangaza matoeko ya kura baada
ya kupigiwa kura akisema kura zote 15 zimeunga mkono hatua hiyo na
azimio ni namba 2162 la mwaka 2014.
Azimio pamoja na kuongeza muda limepongeza ujumbe huo na kazi
zilizofanywa chini ya uongozi wa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Bi
Aichatou Mindaoudou kwa kuchangia kurejesha hali ya usalama nchini humo.
Jitihada zinazohitajika hivi sasa, kwa mujibu wa azimio hilo, ni pamoja
na kubadilisha mfumo wa uraia na umiliki wa ardhi na kutayarisha
uchaguzi unaotakiwa kufanyika Oktoba, mwakani.
UNOCI imepewa mamlaka ya kusaidia serikali ya Cote d'Ivoire katika
maandalizi hayo, baraza la usalama likiwaomba viongozi wa kisaisa
kuachana na maneno ya chuki na kikabila. Halikadhalika walinda amani wa
UNOCI wanatakiwa kupunguzwa, baraza la usalama likitarajia kufunga UNOCI
baada ya uchaguzi wa mwaka 2015, hali ya usalama ikiruhusu.