KUHUSU KUJIUA KAIMU BALOZI WA LIBYA NCHINI, SERIKALI YATHIBITISHA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Baloz...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/kuhusu-kujiua-kaimu-balozi-wa-libya.html
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea
taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi
wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga
risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya
saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa
Lbya.
Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia
risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango
waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka
chini.
Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa
alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho. Maiti
imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat
kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi
hiki kigumu.
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam,
Julai 2, 2014
Dar es Salaam,
Julai 2, 2014