DAKTARI FEKI AMEKAMATWA MANYARA AKIDAI NI DAKTARI WA MAGONJWA YA MOYO
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa ya mkoani Manyara kwa kushirikiana na polisi wamefanikiwa kumnasa mkazi wa jijini Dar-...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/08/daktari-feki-amekamatwa-manyara-akidai.html
Jopo la
madaktari katika hospitali ya rufaa ya mkoani Manyara kwa kushirikiana
na polisi wamefanikiwa kumnasa mkazi wa jijini Dar-es-salaam Bw Godlove
Sozigwa akituhumiwa kuomba kufanya mazoezi ya kutibu kwa muda kama
daktari wa magonjwa ya moyo na figo kwa kutumia vyeti bandia wakati
akitambua kuwa yeye si mtaalam wa tiba.Bw Godlove Sozigwa kabla ya
kukamatwa kwake asubuhi kufuatia jopo hilo la madaktari kubaini kuwa
vyeti alivyoviwasilisha katika hospitali hivyo julai 31 ni bandia na
hata hivyo alipoitwa na kufanyiwa mahojiano amedai huku akionyesha
ukomavu wa kujieleza taaluma hiyo aliipatia katika chuo cha sayansi,
tiba na utafiti cha Muhimbili na kufuzu hata hivyo alibahatika serikali
kumpeleka nchini India kwa mafunzo zaidi kusomea dawa zaidi.
Kwa
upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoani Manyara Dr
Peter Mshali akizungumza na EATV baada ya kukabidhiwa kwa polisi ili
kufanyiwa upelelezi amesema katika mahojiano na jopo la madaktari
walibaini vyeti hivyo ni bandia aidha pia mtuhumiwa Dr huyo Godlove
Sozigwa si mtaalam kulingana na maelezo yake bali ni tapeli na hatari
endapo angebahatika kupata nafasi hiyo.
Naye
kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Deusdedit Nsimeki amekiri na katika
mahojiano amesema polisi imebaini baada ya kumfanyia mahojiano na
upekuzi kumkuta na kompyuta mpakato(laptop) muhuri wa kuchonga wa
hospitali ya rufaa ya Muhimbili, koti na vyeti mbalimbali, lakini
wanafanya upelelezi zaidi kabla ya kumfikisha mahakamani.
Tangu
awali EATV ilishughudia mtego huo mapema asubuhi na baada ya mtuhumiwa
Godlove Sozigwa kufikishwa polisi amekiri kuwa yeye si daktari aliyesoma
chuo hicho cha Muhimbili bali anafanya hivyo kutokana na mazingira
magumu, hasa kwa kuipenda taaluma ya udaktari baada ya kujifunza katika
kituo cha tiba cha Neptune cha matabibu ya kichina kilichopo Ubungo
Plaza jijini Dar-es-salaam na kupata uzoefu.